Ugonjwa wa cirrhosis ni nini?
Cirrhosis ni matokeo ya ugonjwa sugu wa ini ambao hubadilisha tishu za kawaida za ini kwa njia ya fibrosis, scar tishu, matezi (regenerative nodules), kuziba damu kuingia kwenye ini na hivyo kufanya ini kushindwa kufanya kazi yake vizuri.
Visababishi vya ugonjwa huu
Cirhosis husababishwa na mjumuiko wa magonjwa mengi ambayo ni;
- Ugonjwa wa ini unaosababishwa na unywaji wa pombe kupindukia kwa muda mrefu ( alcoholic liver disease) .
Wanywaji pombe kupindukia pia wanaweza kupata tatizo la utapia mlo (malnutrition) kutokana na pombe kukosa virutubisho muhimu vinavyohitajika mwilini, kupungua kwa hamu ya kula, na kupungua kwa ufyonzwaji wa virutubisho vya chakula kwenye utumbo. Utapia mlo pia husababisha ugonjwa wa ini.
Alcoholic hepatitis ni hatari sana kwani unaweza kusababisha kifo.
MAMBO MENGINE YANAYOSABABISHA KANSA YA INI
- Non alcoholic steatohepatitis (NASH) ama Non alcoholic liver cirrhosis – Mafuta hujikusanya kwa wingi kwenye ini na kusababisha huharibifu wa tishu za ini (scar tishu). Ugonjwa huu unahusishwa na kisukari, unene uliopitiliza, utapia mlo wa protini (protein malnutrition), baadhi ya magonjwa ya moyo na baadhi ya madawa aina ya corticosteroids. Mgonjwa hapa hana historia ya unywaji pombe.
- Ugonjwa aina ya hepatitis B, C, na D, ambayo husababishwa na virusi vya hepatitis. Hepatitis B ndio chanzo kikuu cha ugonjwa wa cirhosis kati ya hepatitis zote duniani. Hepatitis C ndio sababu kuu ya wagonjwa wengi kuhitaji ini la kupandikizwa (liver transplant) duniani.
- Autoimmune hepatitis – Husababishwa na mfumo wa kinga mwilini ambao huathiri ini na kuharibu chembechembe au seli za ini na hivyo kusababisha ugonjwa wa cirrhosis.
- Magonjwa ya kurithi kama cystic fibrosis, wilson’s disease, galactosemia, alpha 1 antitrypsin deficiency, hemochromatosis na glycogen storage disease. Watu wenye tatizo la ukosaji wa alpha - 1 -antitrypsin ambayo inakuwa kwenye mapafu ya binadamu na husaidia kukinga tishu zisiharibiwe na enzyme za seli za uhabirifu hasa nuetrophil elastase, wanaweza kupata mjumuiko wa magonjwa yanayoathiri mfumo wa upumuaji (COPD) kama watakuwa na historia ya uvutaji sigara.
- Cardiac cirrhosis - Hutokana na ugonjwa sugu wa moyo unaoathiri sehemu ya kulia ya moyo na hivyo kuufanya moyo kushindwa kufanya kazi yake vizuri na hatimaye kulileletea madhara ini. Husababishwa na tatizo kwenye kizibo cha moyo (valve problem), kuathiriwa kwa moyo na maradhi ya bakteria au virusi, uvutaji sigara na nk.
- Madawa na sumu zinazoharibu na kudhuru ini
- Ugonjwa wa kichocho (schistosomiasis)
- Magonjwa yanayojulikana kama primary biliary cirrhosis na primary sclerosing cholangitis.
- Makala ijayo tutaangalia dalili na viashiria vya cirrhosis.
Post your Comment