JAMANI KANSA YA INI SIKU HIZI INAUA SANA. TUMEAMUA KUANDAA SOMO KAMILI JUU YA GONJWA HILI HATARI.
SOMO HILI LIMEGAWANYIKA SEHEMU TANO.KILA SIKU TUTAZUNGUMZIA SEHEMU MOJA.KARIBUNI.
Ini ni kiungo muhimu sana katika mwili wa binadamu. Ndicho kiungo kikubwa kilichopo ndani ya mwili.
Ugonjwa wa cirrhosis ni ugonjwa wa 12 duniani kati ya magonjwa yanayosababisha vifo vitokanavyo na maradhi.
Cirrhosis husababishwa na unywaji pombe kupindukia, ugonjwa wa hepatitis B, C, na ugonjwa wa fatty liver disease.
Kabla ya kuangalia ugonjwa wa cirhosis (tamka sirosis kwa kiswahili), kwanza tuangalie kazi ya ini kwenye mwili wa binadamu.
Ini linahusika na;
- Kushughulikia chakula kilichosagwa kutoka kwenye utumbo mdogo (small intestine)
- Hulinda mwili dhidhi ya magonjwa
- Kutengeneza nyongo (bile)
- Hudhibiti kiwango cha mafuta, sukari na chembechembe zijulikanazo kama amino acids kwenye damu
- Huhifadhi vitamini, madini ya chuma na kemikali nyengine muhimu
- Huvunjavunja chakula na kutengeneza energy inayohitajika mwilini
- Ini hutengeneza chembechembe zinazozuia damu kuganda mwilini kama fibrinogen, prothrombin, factor V, VII, IX, X na X, protini C na S, antithrombin na nk.
- Huharibu sumu na madawa ambayo yameingia mwilini.
- Hutengeneza homoni aina ya angiotensinogen ambayo inahusika kupandisha presha ya damu mwilini wakati inapokutana na enzyme ya renin, enzyme hii ya renin hutolewa na figo wakati figo inapohisi presha imeshuka mwilini.
- Husafisha damu kutokana na chembechembe mbaya na bakteria.
- Hutengeneza enzyme na protini ambazo zinahitajika mwilini kwenye shughuli nyingi na hata kurekebisha tishu zilizoharibika.
- >>>makala ijayo tutaangazia ugonjwa wa cirrhosis ni nini?
Post your Comment



