Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » "MAFANIKIO NILIYONAYO HAYATEGEMEI MKONO WA MWANAUME".......ODAMA

"MAFANIKIO NILIYONAYO HAYATEGEMEI MKONO WA MWANAUME".......ODAMA

Written By mpekuaji on Wednesday, August 29, 2012 | 4:44:00 AM


Jennifer Kyaka ‘Odama’ amefunguka na kuweka wazi  kuwa katika mafanikio aliyoyapata hakuna mkono wa mwanaume kama ilivyo kwa wasichana wengine mastaa wa mjini.

Odama ameeleza  kuwa amekuwa akifanya kazi kwa bidii na kile anachokipata ndicho anachofanyia mambo yote ya maendeleo ambapo hadi unaposoma hapa, anamiliki kampuni yake ya filamu ya J-Film For Life, magari mawili na mjengo.

“Mafanikio yangu yametokana na kazi zangu mwenyewe na hakuna mkono wa mwanaume, sitaki iwe hivyo ‘coz’ ndiyo maisha niliyoyachagua ya kutomtegemea mtu kwani kile ninachokipata kwenye filamu zangu ndicho kinachonipa maendeleo haya,” alisema Odama.

Hata hivyo, mwanadashosti huyo alisema kwa sasa ana mchumba na anatarajia kufunga ndoa mwakani.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts