Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » Z-ANTO APATA SHAVU LA KUPIGA SHOW YA MWAKA NCHINI ZAMBIA MBELE YA RAIS

Z-ANTO APATA SHAVU LA KUPIGA SHOW YA MWAKA NCHINI ZAMBIA MBELE YA RAIS

Written By mpekuaji on Wednesday, August 29, 2012 | 5:04:00 AM



Msanii wa muziki wa kizazi kipya bongo, hitmaker wa ngoma ya ‘Kisiwa cha Malavidavi’, Z-anto, ameumbia mtandao huu kuwa amepata mualiko mkubwa Wa Serikali ya Zambia kwenda kupiga show nchini humo Septemba 24 mwaka huu huku mgeni rasmi akiwa ni rais wa nchini hiyo .

Msanii huyo alisema kuwa nchi hiyo huwa inasherekea sikukuu yao kila mwaka ingawa hajajua ni sikukuu ya aina gani ingawa kwa taarifa aliyopata ni kuwa siku hiyo wazambia wote huwa hawaendi kazini.


Alisema sasa yupo katika maandalizi ya ishu hiyo ili aweze kuwawakilisha hata wasanii wengine wa Tanzania kwani anaamini safari hiyo haitakuwa ya pekee yake kwani nyuma yake atalibeba taifa la Tanzania.


“Yani ishu ambayo inanisumbua kichwa hapa ni juu ya maandalizi yangu ya safari ya kuelekea nchini Zambia kwa ajili ya kupiga show ambayo mwaliko wake ni mkubwa sana hiyo nawaomba watanzania waniombee niweze kujiandaa vizuri,”
alisema.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts