Mwalimu ni kiungo muhimu sana katika malezi ya wanafunzi hapa nchini.Wao hushinda na watoto wetu kutwa nzima .......
Kwa mantiki hiyo, tabia ya mtoto yeyote aliyewahi kalia madawati ina asilimia zaidi ya 70 ya tabia za walimu wake......
Siku hizi mambo yamebadilika sana.Mwalimu wa miaka ya 90 ni tofauti kabisa na mwalimu wa miaka y leo.
Walimu wa leo wengi wao ni vijana wadogo ambao wengi wamejawa na tamaa za mapenzi.Wao hawajui kutongoza bali wanajua kulazimisha....
Inashangaza na kusikitisha kuona walimu wetu wakishindana KUTOA BIKRA ZA WATOTO WA KIKE......Mtoto akikataa basi cha motoatakiona ....
Mtandao huu umebahatika kuongea na mwanafunzi mmojaambaye ni mhanga wa tukio hilo la kulazimishwa mapenzi na mwalimu wake..........
HILI NI SIMULIZI LAKE:
--------------------------------------------------------------------
"Mwalimu alianza kunitaka tangu nikuwa form one.Nilipomkataa alianza kunichapa tena bila kosa maalumu na kunipa adhabu kila mara...
Baada ya kufanya hivyo kwa muda, aliamua kuniita ofisini na kuniambia kuwa anatanisaidia kimasomo endapo ntamkubalia.Niliamua kumkubali kwa kwa kuhofia viboko na aliniambia nisimwambie mtu.
Siku ya kwanza kufanya mapenzi alinipeleka gesti na aliniambia kuwa atatumia condom.Kwa kuwa ilikuwa ni mara yangu ya kwanza hatukuweza kutumia kinga na alifanya hivyohivyo.
Baada ya hapo tuliendelea kufanya hicho kitendo hata tukiwa shule.Wakati wa kutawanyika, mwalimu alikuwa akiniita katika ofisi yake na kunilazimisha tufanye.....
Miezi kadhaa baadaye, nilianza kujihisi tofauti na wazazi wangu waliyagundua mabadiliko hayo.Walinipeleka hospitali na vipimo vilionesha kuwa nna mimba.Waliponibana ilinibidi niwaeleze ukweli.....
AFISA ELIMU AINGILIA KATI:
Baada ya kubaini hali hiyo, baba alinipeleka moja kwa moja mpaka kwa afisa elimu wa mkoa.Sikuwa na jinsi zaidi ya kueleza ukweli.Mwalimu aliitwa na kuhojiwa.Mwanzo alikataa kabisa lakini baada ya kubanwa ilibidi akubali.
Mwalimu alisimamishwa kazi kwa muda na kufunguliwa mashitaka.Alikaa polisi kwa siku mbili, siku ya tatu alipata dhamana akatoka.....
Alipotoka, mwalimu aliamua kujiua kwa sumu.Shule niliachishwa.nipo nyumbani na mtoto.
--------------------------------------------------------------------
MTAZAMO WETU:
Ni ukweli usiopingika kuwa walimu wa siku hizi wamekuwa ni kero kwa watoto wa kike.Walimu hao hutumia viboko kama msingi wa kuwafanya wakubaliwe maombi yao.Hii ni changamoto kubwa sana inayotukabili sisi wazazi.
Nadhani huu ni wakati mwafaka kwa wanafuni kujitambua na kutokuwa wasiri kwa kuhofia kuchapwa viboko.Waeleze wazazi wako juu ya mkasa unaokukabili maana hayo ndo maisha yako ya baadaye
Post your Comment



