Get the latest updates from us for free

mas template
Home » , , » MABANGO YENYE USO WA RIHANNA ULIOJERUHIWA MWAKA 2009 YATUMIKA KUIPINGA SHOW YA CHRISS BROWN HUKO SWEDEN

MABANGO YENYE USO WA RIHANNA ULIOJERUHIWA MWAKA 2009 YATUMIKA KUIPINGA SHOW YA CHRISS BROWN HUKO SWEDEN

Written By mpekuaji on Monday, November 12, 2012 | 5:51:00 AM



Rihanna anaweza kuwa ameshamsamehe Chris Brown kwa kumpiga miaka mitatu iliyopita lakini kuna watu mjini Stockholm, Sweden bado hawajamsamehe.

Kwa mujibu wa website moja ya nchini Sweden, Alour se, mabango yenye picha ya mpenzi wake wa zamani na Chris zinazoonesha alivyojeruhiwa usoni kutokana na kipigo hicho yamebandikwa kwenye mitaa kadhaa mjini humo kupinga show yake ya November 19.


Chris bado yupo kwenye probation kwa miaka miwili mingine kutokana na kumpiga vibaya Rihanna mwaka 2009. Chris na Rihanna hivi karibuni wamerudisha urafiki wao kiasi cha Breezy kumpiga chini mpenzi wake Karrueche Tran ili tu kuwa karibu na muimbaji huyo wa Diamonds.

Kwa mujibu wa interview ya hivi karibuni kupitia Facebook Live Chat na Andy Cohen Rihanna alisema hana uhusiano wa kimapenzi na Chris.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts