Rais
mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamin William Mkapa amewataka
watanzania kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano kwa kufanya
kazi kwa bidii na kupunguza lawama ili kuonyesha uzalendo aliouacha Baba
wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Rais
Huyo Mstaafu ameyasema hayo katika mkutano wa nane wa Kigoda cha
Mwalimu Nyerere ambao umefanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu
Cha Dar es salaam na kuongeza kuwa watanzania wengi wamekua na desturi
ya kutumia muda mwingi Katika kuilaumu serikali badala ya kufanya kazi kwa maendeleo ya nchi.
"Watanzania
tunatakiwa tufanye kazi kwa bidii ili tuifikishe nchi yetu Kwenye
maendeleo na si kutumia muda mwingi Katika kuilaumu serikali " alisema Dkt Mkapa.
Aidha
Dkt. Mkapa amesema kuwa ili uzalendo uwepo tunatakiwa kutumia vizuri
uhuru wa kuongea Katika kuleta maendeleo na si kuleta uchochezi Katika
nchi na kusababisha uvunjifu wa amani ambayo ameiacha Mwal. J.k nyerere.
Mbali
na mkutano huo pia kulikua na uzinduzi wa kitabu cha uchumi wa kisiasa
wa mabadiliko ya Tanzania kijulikanacho kama (political economy of
change in Tanzania) ambacho kina lengo la kukuza uchumi na siasa nchini.
Mkutano
huo wenye lengo la kudumisha uzalendo na kukuza uchumi nchini
umehudhuriwa na wawakilishi Mbali Mbali wa kitaifa na kimataifa wakiwemo
baadhi ya mabalozi na wanazuoni kutoka ndani na nje ya nchi.
Kwa
upande wa Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Prof. Rwekaza
Mukandala alisema kuwa mkutano huo unalenga kudumisha na kuendeleza
aliyoyaacha Baba wa Taifa Hayati Mwl. J.k Nyerere.
Mbali
na hayo amewataka vijana na watanzania kwa ujumla kumuenzi kwa kufanya
kazi kwa bidii ili kujikwamua kiuchumi na kuendeleza ujamaa aliouacha
Mwalimu.
Post your Comment



