Bodi ya ushauri ya kupambana na rushwa na ufisadi barani
Afrika (AUABC) imeelezea kurishwa kwake na hatua zinachukuliwa na
serikali ya Tanzania kupambana na vitendo hivyo na imewataka viongozi
wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU)kuiga mfano wa Rais wa
Tanzania Mh Dr. John Magufuli wa kuonyesha kwa vitendo yale
wanayozungumza kwenye majukwaa.
Mwenyekiti wa bodi hiyo Bw Daniel Batidam amewaambia waandishi wa
habari jijini Arusha kuwa kwa sasa asilimia kubwa ya wananchi
wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU)wanamuona Rais wa Tanzania Mh
Dr John Pombe Magufuli kama mfano wa kuigwa kutokana na msimamo wake wa
kuonyesha vitendo zaidi kuliko maneno katika kukabiliana na
rushwa,ufisadi na pia kusimamia uwajibikaji.
kuhusu hali ya rushwa na ufisadi katika nchi za afrika Bw.Batidam
amesema pamoja na jitihada za taasisi mbalimbali za kupambana na
vitendo hivyo tatizo bado ni kubwa na linaendelea kuwaathiri wananchi
wengi hasa wa kipato cha chini.
Baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo kutoka nchi kumi na moja za Umoja
wa Afrika waliokutana Arusha wamesema ili tatizo la rushwa na ufisadi
liweze kupata ufumbuzi wa kudumu linahitaji ushirikiano mkubwa zaidi
hasa kutoka kwa wananchi.
Katika kutambua mchango wa Tanzania katika masuala ya kukabiliana
na maovu mbalimbali nchi za umoja wa afrika zimeridhia makao makuu ya
taasisi hiyo ya African Union Advisory Board on Corruption
(AUABC)kujengwa Arusha Tanzania na mradi ambao unatarajiwa kuanza
wakati wowote kuanzia sasa.
Post your Comment



