Baada ya kuachana na Shilole na kumwagana pia na aliyekuwa mchumba wake
mwenye asili ya kiarabu Erah,Nuhu Mziwanda ameamua kupoza moyo wake kwa
mpenzi mpya ambae amemchora tatoo.
Akizungumza
na Enewz Nuhu alisema kuwa anamshukuru mungu kwasababu mwanamke aliye
nae ni mwanamke ambae amemuonyesha upendo kwa muda mfupi sana na
anamuomba mungu kila siku amuweke kipenzi chake huyo na awe na moyo huo
huo wa kumpenda zaidi.
Akizungumzia tatoo aliyochorwa na mwadada huyo Nawary, Nuhu alisema
kuwa ni upendo wa hali ya juu ulioonyeshwa na msichana huyo baada ya
yeye nae kumuonyesha upendo wake wa kweli na kudai kuwa hawajali watu
wanazungumza nini juu yao ila yeye anampenda,anamuheshimu na hatoweza
kumuangusha kamwe.
Post your Comment




