Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) katika kuhakikisha elimu na uhiari
wa wananchi kupenda kulipa kodi unaongezeka nchini wameendeleza jitihada
zake za kuanzisha jumuiya za wanafunzi wa kodi vyuoni ili kuandaa
vijana waweze kutimiza wajibu wao pindi watakapoanza kupata mapato.
Akizungumza katika ufunguzi wa jumuiya ya wanafunzi wa kodi vyuoni
katika chuo cha kodi, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi,
RICHARD KAYOMBO, amesema hatua hiyo ni baada ya kuanzisha mfumo wa
vilabu vya kodi kwenye shule za sekondari kuonesha mafanikio hivyo
mamlaka ya mapato ikaona umuhimu wa elimu hiyo kufika katika ngazi za
vyuo ili kutoa fursa kwa wanavyuo kuweza kujadili mambo mbalimbali ya
kodi wakiwa katika mazingira yao ya vyuo.
Jumuiya hizo zinapaswa kuhakikisha zinaongeza uelewa na uhiari wa
wananchi kupenda kulipa kodi pamoja, taratibu na sheria za kodi
kueleweka vyema kwa jamii pamoja na kuongeza wigo wa kodi kwa kuibua
vyanzo vipya vya kodi, huku Mamlaka ya Mapato Tanzania ikiwa na majukumu
ya kutoa elimu ya kodi kwa wanachama ili waweze kuelewa sheria za kodi
zinazosimamiwa na mamlaka ya mapato Tanzania pamoja.
Post your Comment



