Makatibu
wakuu wa wizara za Mawasilino, Elimu na TAMISEMI nchini Tanzania
wamezitaka mamlaka husika ikiwemo ya jeshi la polisi kumbaini mtu
aliyesambaza taarifa walizodai ni za upotoshaji zinazosema kuwa ajira za
ualimu kwa mwaka 2015-2016 zimesitishwa.
Wakizungumza kwa pamoja leo jijini Dar es salaam makatibu hao
wamesema taarifa hizo zilizopo kwenye mitandao ya kijamii zina lenga
kuleta chuki baina walimu hao na serikali, jambo ambalo ni lazima
wahusika watafutwe na kuchukuliwa hatua.
Akizungumza katika mkutano huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Faustini Kamuzora amesema wizara yake
imeanza kulifanyia kazi suala hilo na itahakikisha aliyehusika kusambaza
taarifa hizo za uongo anabainika na kuchukuliwa hatua.
Amesema sheria ya makosa ya mitandao ndiyo itatumika katika kumtafuta
na kumkamata huku akisisitiza kwa watumiaji wa mitandao kuitumia
teknolojia hiyo kwa malengo mazuri na sio vinginevyo.
Post your Comment



