Msanii wa RnB Abednego Damian ‘Belle 9’, amesema umaarufu wa mkali wa
kunogesha video za wasanii, Agnes Gerald ‘Masogange’, umetokana na wimbo
wake wa ‘Masogange’.
Belle 9 alisema huwa anaamini kipaji cha mtu ndio maana wengi aliowashirikisha katika nyimbo zake wamepata umaarufu mkubwa.
“Nimefanya kazi na wasanii wasiotambulika akiwemo Masogange na
wamepata umaarufu mkubwa pia nimefanya kazi na maprodyuza wengi
wasiojulikana lakini baada ya kazi hizo wamejulikana, hivyo huwa
sidharau uwezo wa mtu ninachoangalia ni ubora wa kazi zake na si jina
lake hata kama ni chipukizi,” alisema.
Post your Comment


