Zari Hassan maarufu kama Zari the
Bossylady kutoka Uganda, na mzazi mwenza Diamond Platnumz a.k.a Chibu
Dangote ambaye ni mwanamuziki wa kizazi kipya kutoka hapa nchini,
Amezuiliwa kuendesha event yake ya ‘Zari All White Party’ hapa nchini
Tanzania na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa kile kinachosemekana
kwamba hakutimiza masharti aliyowekewa kabla ya kufanya event hiyo mara
ya mwisho kufanyika hapa Dar es salaam.
Zari alianza kufanya matangazo ya event
yake kabla ya hajakamilisha taratibu zote za BASATA mnamo mwaka 2014, na
kwa kosa hilo alipewa faini ya kiasi cha fedha TZS 460,000/- na
kuzuiliwa kufanya event hiyo hapa nchini mpaka atakaporuhusiwa, na hiyo
ni endapo atafata kanuni na taratibu zote alizowekewa na Baraza la
Sanaa.
Post your Comment



