Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John
Kijazi anapenda kuwataarifa wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,
Miji na Wilaya walioteuliwa tarehe 07 Julai, 2016 kuwa watakapofika Ikulu Dar
es salaam kwa ajili ya kula kiapo cha uadilifu wa uongozi wa umma siku ya
Jumanne tarehe 12 Julai, 2016 wahakikishe wanakuja na nakala zao halisi za
vyeti vya kitaaluma (Original Academic Certificates).
Ieleweke kuwa uhakiki wa vyeti
halisi vya kitaaluma (Original Academic Certificates)
unafanywa kwa lengo la kujiridhisha baada ya mchakato wa kawaida wa uhakiki
kufanywa kwa kutumia vyeti visivyokuwa halisi (Photocopies).
Uhakiki huu wa vyeti utaanza saa
mbili asubuhi na wahusika wote mnaombwa kuingia Ikulu kwa kupitia geti kuu la
lililopo upande wa mashariki (Upande wa
Baharini)
Tafadhali zingatia maelekezo
haya.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa
Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
09 Julai, 2016
Post your Comment


