Mwanamuziki nguli wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Koffi
Olomide amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela huko DRC kwa kumpiga
teke mmoja wa madansa wake aitwaye Pamela akiwa nchini Kenya.
Nguli huyo wa muziki wa Rhumba amehukumiwa muda mfupi baada ya kukamatwa na polisi akiwa nyumbani kwake mjini Kinshasa.
Koffi alikana tuhuma za kumpiga dansa huyo na mwanasheria wake
aitwaye George Wajackoyah naye amelaani kitendo cha polisi kutumia nguvu
kubwa wakati wa kumkamata staa huyo.
Staa huyo alikamatwa nchini Kenya Ijumaa iliyopita na kurudishwa DRC
kesho yake asubuhi baada ya video yake kusambaa mitandaoni ikimuonesha
akimpiga teke mmoja wa madansa wake aitwaye Pamela mara baada ya
kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Jomo Kenyatta (JKIA) kwa
ajili ya tamasha.
Koffi anadaiwa kufanya tukio hilo baada ya Pamela kukorofishana na
mwanamuziki wake aitwaye Cindy Le Couer anayedaiwa kuwa ni mpenzi wa
Koffi.
Post your Comment



