Kaburu (wa kwanza kulia) akiutambulisha uongozi wake mpya wa Kaburu Record
Uongozi wa ‘Kaburu Records’ studio ya kisasa iliyozinduliwa
miezi mitatu iliyopita na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi,
imemtimua aliyekuwa meneja wa studio hiyo Msafiri Peter ‘Papa Misifa’
kwa madai ya kushindwa kufikia malengo ya kampuni hiyo.
Akiongea Jumanne hii, Mmiliki wa studio hiyo, Kaburu,
amesema wameamua kuachana na bosi huyo wa zamani wa Diamond na Rich
Mavoko kutokana na kushindwa kuifikisha kampuni hiyo sehemu ambayo
waliafikiana.
“Kaburu Record kama kampuni tumeamua kumsimamisha kazi Msafiri Peter
‘Papa Misifa’ kutokana na kushindwa kuifikisha kampuni yetu sehemu
ambayo tulipanga,” alisema Kaburu. “Miezi mitatu sio mingi toka
tumtangaze lakini kama kampuni kuna vitu ambavyo tulivipanga kuvifanya
ndani ya muda huo lakini mpaka sasa hakuna dalili yoyote ya utekelezaji,
hii ni biashara tumewekeza pesa ili izalishe taratibu lakini tumeona
imeshindikana,”
Aliongeza, “Kwa hiyo mimi kama mtu kwenye hisa kubwa kwenye kampuni
hii nimeamua kumfuta kazi na kuweka uongozi mpya, Papa Misifa hayupo
tena kwenye kampuni hii, ukitaka kufanya kazi na sisi njoo ofisini,”
Post your Comment



