Meneja wa Snura, HK amedai kuwa hata kama serikali wakiikataa script ya
video ya ‘Chura’ waliyoipeleka ikikataliwa bado wataendelea kupeleka
nyingine.
Akiongea nasi, HK amesema, “Hata wakiikataa hii script ya pili tutawapelekea script nyingine.”“Tumeshapeleka script nyingine zaidi ya wiki tatu zilizopita na
nimewapigia simu jana wameniambia bado hata kuipitia bado hawajaipitia.
Tulikubaliana na serikali kuwa ni lazima video ya ‘Chura’ ifanyike,”
alisema HK.
“Script tuliyowapelekea ni ya kawaida sana, kama wataikataa itabidi
tuziweke zote mbili hadharani ili watu wachangie kwa kuwa hata ile ya
kwanza haikuwa mbaya, walisema kuwa haina ujumbe kwahiyo kwenye script
ya sasa hivi tumezingatia maamuzi yao waliyoyataka kwenye script hiyo,”
ameongeza.
Hivi karibuni Snura ameachia wimbo wake mpya ‘Shindu’ ambao unazidi kufanya vizuri kwenye redio na mitaani pia.
Post your Comment



