Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Msumbiji Mheshimiwa Filipe Nyusi.
Ujumbe
huo uliwasilishwa jana jijini Dar es Salaam na Mjumbe Maalum wa Rais
Nyusi Meja Jenerali Mstaafu Mariano de Araujo Matsinhe ambaye
aliongozana na Mshauri wa Diplomasia wa Rais Nyusi Kanali Manuel Mazuze,
Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania Mheshimiwa Monica Patricip Clemente
Mussa na Afisa wa Ubalozi wa Msumbiji nchini Rachide Usualle.
Post your Comment