Huenda Miss Tanzania wa zamani, Happiness Millen Magese
siku za usoni kama Mungu akipenda akawa na furaha kama ya wanawake wengi
duniani – furaha ya kupata mtoto.
Ni kwasababu tatizo lake la Endometriosis limemuondolea matumaini ya
kuwa mama lakini sasa inaonekana kuwa matumaini yamerejea, shukrani kwa
sayansi ya IVF.
Kwa mujibu wa post aliyoiweka Instagram, huenda Millen akawa
amefanyiwa mchakato huo May 13 na hivyo siku za usoni anatarajiwa kuwa
mama.
“Sijawa mama tayari lakini ninakikumbatia kila kitukilichoongezwa kwenye mwili wangu na kwenye maisha yangu kwa ujumla tangu May 13,” inasomeka sehemu ya post aliyoiweka inayomuonesha kwenye video akitembea kwa furaha kwenye ufukwe wa bahari
Post your Comment