Mwandishi
Mwandamizi wa Habari za michezo na burudani wa gazeti la Majira,
Elizabeth Mayemba amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuanguka ghafla
nyumbani kwake eneo la Tabata kwa Swai jijini Dar es Salaam.
Taaifa
za awali zinaeleza kuwa, tukio hilo limetokea majira ya saa mbili usiku Julai 9.2016,ambapo inaelezwa alikuwa akijisikia kizunguzungu,ghafla alianguka chini na
ndipo alipopatwa na umauti huo licha ya kukimbizwa Hospitali.
Aidha,
Taarifa kutoka kwa mume wa marehemu, Eliza, Bwana Rogers amebainisha
kuwa…, alipigiwa simu saa mbili usiku na kuambiwa Eliza alisikia
kizunguzungu ghafla na kuanguka chini, alichukuliwa na kupelekwa
hospitali baada muda mtu aliyempeleka Eliza hospital alimpigia tena na
kumpa taarifa za Eliza kufariki.
Taarifa nyingine zitatolewa baada ya ndugu wa marehemu kukutaana.
Chanzo chetu kinatoa pole kwa ndugu na jamaa wote popote pale walipo. Ni pigo kubwa katika tasnia ya Habari.
Post your Comment


