Mtu mmoja mwanaume ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 mpaka 40
jina halijafahamika, ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali
kichwani na kupigwa hadi kufa na wananchi wenye hasira baada yakumkamata
akifanya kitendo cha wizi wa kuku Mtu huyo aliyepigwa na marungu, alifanya kitendo hicho kipindi cha sikukuu ya Eid.
Taarifa ya tukio hilo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza
Ahmed Msangi kuhusu matukio
yaliyojitokeza kipindi cha sikukuu ya Eid na sikukuu ya Sabasaba, na
kusema tukio hilo limetokea baada ya mtu aliyeibiwa kuku hao kuomba
msaada kwa wananchi na wananchi kumkamata mwizi huyo na kuanza kumpiga
na silaha hizo mpaka kumsababishia mauti.
Kamanda Msangi amesema jeshi la polisi mkoani humo linawashikilia
watu watatu kwaajili ya mahojiano ya tukio hilo na kuwataka watanzania
kuacha kufanya vitendo vya kihalifu kwa kisingizio cha kukosa ajira za
kuwaingizia kipato cha kila siku, kwani vitendo hivyo vya kihalifu
vinagharimu maisha yao na kuwasababishia kifo.
Amewaasa watanzania kuacha kujichukulia sheria mkononi na watumie vyombo vya usalama katika kupambana na wahalifu.
Post your Comment


