Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye baada ya kufanya ziara Ijumaa hii katika maeneo ya Kariakoo kukagua na kukamata CD ambazo hazina stika ya TRA, amewataka watanzania kuacha tabia ya kukunua CD ambazo hazina stika za TRA.
Akiongea na waandishi wa Habari katika msako huyo, Nape amesema
yeyote anayekamatwa na CD ambao haina stika ya TRA atashtakiwa kwa kosa
la kuhujumu uchumi.
“Kila anayenunua sasa kazi ya sanaa ambayo haina stika ya TRA naye ni
mwizi kwa kama mwizi yoyote sababu ameshirikiana na muuzaji ambaye
hajalipa kodi, hata tukikukuta na CD moja haina stika wewe ni mwizi kama
mwizi mwingine tutashughulika na wewe,” alisema Nape.
Katika ziara hiyo zaidia ya maduka 40 yamefungwa huku CD fake zikichukuliwa kwa ajili ya kuaribiwa.
Post your Comment



