Msanii Roma Mkatoliki amefunguka na kusema kuwa ataendelea kuichana
Serikali pale ambapo inakosea na wataisifia pale inapotenda mambo mema
kwa jamii na amesisitiza kuwa yeye anaamini kuwa mpaka sasa katika
uongozi wa Rais Magufuli kuna mambo mengi ya kuzungumza au ya kuimba kwani kuna matukio mengi yaliyotokea ambayo jamii inataka majibu yake.
“Tutaendelea kuichana Serikali pale inapokosea na itasifiwa pale
inapofanya mambo ya msingi kwa jamii, ila mpaka sasa kuna mambo mengi ya
kuimba kwenye uongozi huu, hata jamii nayo inaposikia nataka kutoa kazi
watu wanaanza kujiuliza, mambo kama bunge live, Sukari, hivyo kunamambo
mengi sana ya kuimba” alisisitiza Roma Mkatoliki.
Roma Mkatoliki amesema kuanzia sasa muda wowote ataachia wimbo wake
mpya unaoitwa ‘Kaa Tayari’ hivyo watu wasubiri kusikia ndani ya wimbo
huo ameimba nini.
Post your Comment



