Mkuu wa Wilaya (DC) Mteule wa wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya, Ally
Masoud Maswanya ametangaza kujiondoa katika nafasi hiyo ya ukuu wa
wilaya.
Kufuatia kujiondoa huko kwa Ally Masoud, aliyekuwa mkuu wa wilaya ya
Kongwa, John Ernest Palingo anakwenda kuwa mkuu wa wilaya ya Mbozi, na
Kongwa itasubiri uteuzi mpya utakaofanya na Rais Magufuli.
Sababu ya kujiondoa katika nafasi hiyo bado haijawekwa wazi lakini
watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Tanzania wamekuwa wakisema
maslahi ya kifedha ya utumishi wa umma kama Mkuu wa Wilaya ni madogo
ukilinganisha na nafasi yake katika kampuni ya Tigo ambapo wastani wake
wa mshahara kwa mwezi ni zaidi ya shilingi milioni 10 za Kitanzania
pamoja na faida nyingine nyingi katika taaluma yake.
Post your Comment



