Hayawi hayawi sasa yamekuwa. Baada ya miaka mingi ya uhusiano thabiti na
uliokuwa umetawaliwa na upendo usio kifani, Mwenyekiti Mtendaji wa
Bongo5 Media Group Limited, Luca Neghesti na Miss Tanzania 2005 na Miss
World Africa, Nancy Sumari wamefunga ndoa Ijumaa hii.
Luca na Nancy wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kike, Zuri.Wawili hao wamefunga ndoa jijini Arusha na kuhudhuriwa na watu takriban
60 ambao wengi wao ni ndugu na marafiki zao wa karibu. Tunawapongeza kwa
hatua hiyo kubwa kwenye maisha yao.
Post your Comment






