Serikali kupitia wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi imefuta
maadhimisho ya wiki ya elimu nchini badala yake imezindua mpango wa
kuimarisha shule zote kongwe zilizoweza kuzalisha wataalamu mbalimbali
ili kuendelea kukuza elimu na kurudisha sifa na uwezo wa shule hizo.
Mpango huo unaolenga kukuza elimu nchini umezinduliwa mkoani
Morogoro na waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Prof.Joyce Ndalichako
wakati wa utoaji wa zawadi kwa wanafunzi, shule, halmashauri na mikoa
iliyofanya vizuri kwenye masomo na kupata ufaulu wa hali ya juu ikiwa
ni sehemu ya kutoa motisha ambapo ametoa zawadi za fedha taslimu vyeti
na tuzo kwa shule hizo ambapo katika mikoa na halmashauri zilizofanya
vizuri kitaifa zimeongozwa na mkoa wa Katavi huku akibainisha wiki ya
elimu ambayo imefutwa rasmi ilikuwa ikisababisha upotevu wa fedha nyingi
kutokana na takribani bilioni 1.2 kutumika katika maadhimisho hayo
badala yake sasa fedha hizo zitaelekezwa kuboresha miundombinu katika
shule zote nchini kwa kuanza na shule zote kongwe.
Mkurugenzi wa usimamizi wa elimu kutoka TAMISEMI Mwl.Juma Japhet
amesema wako tayari kushirikiana kikamilifu na wizara hiyo katika
kuboresha miundombinu ya shule na kutatua changamoto za walimu nchini
huku mkuu wa shule ya sekondari ya Mzumbe ambayo ni miongoni mwa
zilizopata tuzo, alikiri kuwepo kwa changamoto ya miundombinu na vifaa
ingawa akataja mbinu wanazotumia kufanikisha kutoa elimu bora.
Post your Comment



