Katika hotuba yake kuadhimisha miaka 50 ya Benki Kuu ya Tanzania,
Rais John Pombe Magufuli amewatoa hofu wafanyakazi wa serikali kwa hatua
ya kusitisha ajira serikalini kwa muda akielezea sababu kuu mbili za
kuchukua uamuzi huo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
amesema serikali imeamua kusimamisha kwa muda mfupi usiozidi miezi
miwili zoezi la utoaji ajira mpya na upandishaji wa vyeo kwa watumishi
wa umma kwa lengo la kupisha uhakiki wa watumishi wa umma katika orodha
ya malipo ya mshahara na kuondoa watumishi hewa.
Rais Magufuli amesema hayo leo tarehe 22 Juni, 2016 katika Jubilei ya
miaka 50 ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) iliyofanyika katika ukumbi wa
Benki hiyo, Mtaa wa Mirambo Jijini Dar es salaam.
Post your Comment



