Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli amewataka wanasiasa kuachana na
harakati za siasa katika kipindi hiki mpaka baada ya miaka mitano ili
kutoa nafasi ya kutekeleza ahadi alizozitoa kwa ajili ya Maendeleo na
Watanzania na nchi kwa ujumla.
Akizungumza
leo Ikulu Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amewataka wanasiasa
waliopewa nafasi za uwakilishi na wananchi wajikite zaidi katika
kuwahudumia ili kuwaletea maendeleo waliyowaahidi wakati wa kampeni.
Rais Magufuli amesema kuwa wakati wa uchaguzi umekwisha hivyo wakati
wa siasa sasa nao umekwisha hivyo amewataka viongozi wao wa siasa
kushirikiana nae katika kuleta maendeleo ikiwemo kumpa ushauri ambao nae
ataufanyia kazi kwa maendeleo ya Wananchi wote.
Dkt. Magufuli amesema kuwa kamwe hatomvumilia mtu yoyote ambae
atamchelewesha katika harakati zake za kuwaletea maendeleo wananchi,
hivyo ni vyema wakaungana kwa pamoja katika kufanikisha suala hilo.
Rais Magufuli amesema wabunge waliochaguliwa waelekeze nguvu katika
kuwasemea wananchi kwa kufuata demokrasia ingawa hata kuziba midomo ni
demokrasia ya aina yake lakini amevitaka vyama vyote kushirikiana nae
katika kulileta taifa maendeleo.
Post your Comment



