Msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, Judith Mwangi ‘Avril’ ambaye
alicheza kama video queen kwenye wimbo wa Diamond Platnumz ‘Kesho’
amefunguka na kusema hakuwahi kutoka kimapenzi na Diamond Platnumz kama
ambavyo baadhi ya watu walivyokuwa wakidhani huenda kuwa Diamond
Platnumz baada ya video hiyo labda alitumia nafasi hiyo kutoka naye
kimapenzi.
Avril alisema
kuwa yeye na Diamond Platnumz hawakufanya project nyingine yoyote zaidi
ya kutengeneza video ile ya ‘Kesho’ japo alimuelezea Diamond kuwa ni
msanii mpole sana na mwenye kupenda kazi yake na kujituma.
“Diamond ni rafiki yangu ni mtu poa sana, tumejuana kwa muda mfupi
lakini ni msanii mwenye bidii ya kufanya kazi na kukutana na msanii
mwenye bidii ni jambo zuri, hi mtu mzuri mpole hana maneno na watu.
Najua vyombo vya habari vinampa sifa nyingi tofauti na yeye lakini
ukikutana na yeye moja kwa moja ni mtu mzuri sana. Baada ya kufanya ile
video ya kesho hakuna project nyingine tulifanya” alisema Avril
Mbali na hilo Avril alitaja wasani watano kutoka Tanzania ambao
anawakubali na kuanza na Diamond Platnumz, Ommy Dimpoz, Raymond, Vanessa
Mdee pamoja na Linah Sanga.
Post your Comment



