Baadhi ya waaandaaji wa Filamu nchini waanza kujisalimisha Bodi ya
Filamu Tanzania baada ya Filamu zao kukamatwa zikiwa sokoni wakati
hazijafanyiwa uhakiki na Bodi hiyo.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania
Bibi. Joyce Fissoo alipokuwa akifanya mahojiano na mmoja wa waandaaji wa
Filamu nchini aliyekutwa na kadhia hiyo Bw. Akim Igembe kutoka Kampuni
ya Akim Master Film baada ya Filamu yake ijulikanayo kwa jina la
“Mapenzi Uchizi” bango lake lilikutwa sokoni likiwa na alama ya Uhakiki
kutoka Bodi ya Filamu wakati ilikuwa bado haijahakikiwa na Bodi hiyo.
“Operesheni ya kukamata Filamu zilizoingizwa sokoni kinyume cha
sheria ambayo ilimshirikisha na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Nnauye ki ukweli imekuwa ya mafanikio sana maana sasa
wameanza kujileta wenyewe.”Alisema Fissoo
Aliongeza, “Wakati tunapitia fomu ya Uhakiki wa Filamu hii tulibaini
kuwa ni moja kati ya kazi tulizozikamata kutokana na kuwa na alama ya
uhakiki bila kupitia kwetu, tena ikiwa na daraja 18 wakati katika daraja
hali la filamu hiyo inapaswa kuwa ni daraja 16,”
Katika hatua ngingine, Mwenyekiti wa Chama cha Wasambazaji wa Filamu
Tanzania, Moses Mwanyilu amepongeza hatua iliyochukuliwa na Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo kupitia waziri wake, Nape Nnauye
katika kuhakikisha wanatokomeza waharamia na uuzaji wa kazi za wasanii
bila kufuata utaratibu za kisheria zilizowekwa.
Post your Comment



