Get the latest updates from us for free

mas template
Home » » Wakurugenzi wote,Mameneja na Mhandisi wa NSSF wametumbuliwa na wanne kati yao wako chini ya ulinzi.

Wakurugenzi wote,Mameneja na Mhandisi wa NSSF wametumbuliwa na wanne kati yao wako chini ya ulinzi.

Written By Vuvuzela on Tuesday, July 19, 2016 | 6:53:00 AM


BODI ya wakurugenzi ya Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limewasimamisha kazi wakurugenzi sita,meneja watano na Mhandisi mmoja kufuatia matumizi mabaya ya ofisi na kutofuata sheria na kanuni.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugnezi Mkuu wa NSSF,  Profesa Godius Kahyarara imesema hatua ya kuwasimamisha kazi wakurugenzi na mameneja hao inafuatia kikao cha bodi chini ya uenyekiti wa  Prefesa Samweli Wangwe kilichokaa kuanzia Ijumaa iliyopita.

“Bodi imeagiza  kusimamishwa kazi Wakurugenzi, Mameneja watano na Mhandishi mmoja ili kupisha uchunguzi ili kubaini wahusika katika tuhuma za ubadhirifu, matumizi mabaya ya ofisi na kutofuata kanuni, sheria na utatibu katika uwekezaji,  usimamizi wa miradi na manunuzi ya ardhi na ajira,” alisema Profesa Kahyarara.

Aliwataja wakurugenzi hao ni Mkurugenzi wa mipango, Uwekezaji na Miradi, Yakub Kidura, Mkurugenzi wa fedha, Ludovick Mrosso, Mkurugenzi wa rasilimali watu na utawala, Chiku Matessa, Mkurugenzi wa Udhibiti,Hadhara na Majanga, Sadi Shemliwa, Mkurugenzi Mahesabu ya ndani, Pauline Mtunda na Mkurugenzi wa Uendeshaji,  Crescentius Magori.

Aidha Aliwataja mameneja waliosimamishwa ni pamoja na Meneja wa utawala, Amina Abdallah, Meneja wa Uwekezaji, Abdallah Mseli, Meneja Miradi, Mhadisi,John Msemo, Mhasibu Mkuu, Davis Kalanje, Meneja kiongozi mkoa wa Temeke, Wakili,  Chedrick Komba na Mhadisi John Ndazi.

Awali amedaiwa kuwa baadhi ya wakurugenzi na mameneja waliosimamishwa,jana  wamefikishwa katika kituo cha polisi cha kati Dar es Salaam kwa mahojiano kufuatia tuhuma hizi zinazowakabili.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts