Diamond Platnumz anazidi kuwa karibu tena na maex wake. Jacqueline
Wolper, Wema Sepetu hawana noma naye tena – na sasa Jokate Mwegelo!
Ya Jokate ina nguvu zaidi kwakuwa kwa sasa ana uhusiano na hasimu
wake kiburudani, Alikiba na hiyo ni ishara kuwa uadui kati ya Diamond na
Kiba umebaki kwa mashabiki tu.
Mrembo huyo amempongeza Diamond kwa uwezo wake mkubwa wa uchezaji wa style mpya kwenye hit single yake, Kidogo.
Akipost kipande cha video Instagram kikimuonesha Diamond na dancers
wake wakifanya mazoezi kwa wimbo huo, Jokate ameandika: You just took
choreography ya East African tracks to another sphere, inspirational is
an understatement. Moves za kwenye huu wimbo. I can’t even hata.”Jojo pia anatamani amuone Chibu na Kiba kwenye ngoma moja.
“Naendelea kusubiri siku utakayo fanya kazi na team kiba tho- kiroho safi.Hongera kwa kazi nzuri dogo @diamondplatnumz.”
Mapokezi ya post hiyo yana mchanganyiko wa hisia. Ila wengi wamempongeza.Mara ya mwisho Jokate anamuongelea Diamond ilikuwa ni malalamiko aliyommwagia kwa kumuita mswahili na mdhalilishaji wa wanawake.
Post your Comment