Mkali wa muziki wa R&B Bongo, Ben Pol amedai kuwa muziki umempa
heshima kubwa kwenye maisha yake kwa kuweza kuisaidia familia yake.
Wimbo wa ‘Moyo Mashine’ wa Ben Pol umezidi kufanya vizuri kwenye Radio na TV kubwa Afrika.Muimbaji huyo ameiambia BBC Radio kuwa kwa sasa muziki umemsaidia kusomesha wadogo zake wawili kwenye shule nzuri.
“Wadogo zangu wapo wawili nimewatoa shule ambazo naona siyo nzuri
nimewapeleka shule nzuri wanasoma nina wahudumia kila kitu. Wazazi wangu
sasa hivi wameshakuwa watu wazima kidogo ufanisi umepungua mimi ndio
nipo responsible,” amesema Ben Pol.
Aidha staa huyo ametoa sababu ya kuupa wimbo wake mpya jina la ‘Moyo
Mashine’ ni kutokana na moyo umekuwa ukifanya kazi kubwa kwenye mwili
kama mashine.
Post your Comment