Tanzania imeendelea kuwa na neema
ya kutembelewa na viongozi wa mataifa mengine baada ya usiku wa kuamkia
leo Jumapili Waziri Mkuu wa India, Mhe. Narendra Modi kuwasili nchini
ambapo alipokelewa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na viongozi
wengine wa kitaifa na kimkoa Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Mhe. Paul Makonda akisalimiana na Mhe. Modi mara baada ya kuwasili
katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Post your Comment




