Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu ameonesha kuchoka na maneno
mbalimbali kutoka kwa watu hususani kwenye mitandao ya kijamii kiasi cha
kuamua kutoa yake ya moyoni kwa watu wote ambao wamekuwa wakimfuatilia
maisha yake.
Ameonesha kukasirishwa na baadhi ya watu wanaomsema kwenye mitandao ya kijamii hususani kuhusu mapungufu yake.
Wema Sepetu ametumia mtandao wake wa Instagram kuweka ujumbe mrefu
kwa watu hao, huku akiwataka wamuache aishi maisha yake kwani hajawahi
hata siku moja kwenda kuomba msaada kwao, na kusema hata siku
atakapokufa atakufa mwenyewe na kama ni majibu kwa Mungu atajibu
mwenyewe.
"Naomba niseme kitu na nieleweke tafadhalli, sijawahi hata siku moja
kwenda kwa hata mmoja wenu na kumgongea kuomba hata hela ya chumvi.
Maisha yangu yananihusu mimi na hata siku nikifa nakufa mwenyewe, majibu
kwa Mungu naenda kujibu peke yangu. Niacheni jamani nimechoka"
aliandika Wema Sepetu
Mbali na hilo Wema Sepetu amewataka watu ambao wanakereka na aina ya
maisha ambayo yeye anaishi waache kuyafuatilia kwani si lazima
kufuatilia kile akifanyacho au maisha anayoishi yeye.
"Kama nakukera na maisha yangu basi usiyafuatilie siyo lazima.
Nisiheme sasa jamanii. Naomba tafadhari kama mapungufu ni ya kwangu
mimi. Niacheni mimi nafanya kile kinachoridhisha nafsi yangu maana
sipendi kujikasirisha. Kwani nikitajirika mimi au nikiwa masikini wewe
unapata faida gani. Jiulize kwanza hilo swali ndiyo uanze kutoa maneno
yako" alisema Wema Sepetu
Post your Comment




