Malkia wa filamu Wema Sepetu bado hajakata tamaa kuhusu kupata mtoto
licha ya kukatishwa tamaa na baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii
kutokana na uzazi wake kuwa mgumu.
Muigizaji huyo ambaye alianzisha mfumo wa APP na SMS ambao unatoa
taarifa zake mbalimbali kwa mashabiki juu ya maisha yake, tayari umeanza
kutoa taarifa mbalimbali kuhusu maisha yake.
Kupitia mfumo huo, Wema amesema angependa mwanae wakiume ampatie jina la Karma.
“Mtoto wangu wa kiume ataitwa Karma,” alisema Wema. “Bado sijafikiria
jina nitakalo mpa mtoto wangu wa kike japo namtaka sana mtoto wa
kwanza awe wa kiume, Mungu anajua,” alisema Wema.
Pia kupitia system hiyo, Wema amewashukuru mastaa wenzake wa filamu ambao walimsupport katika show yake ya ‘The Black Tie’.
Post your Comment