Get the latest updates from us for free

mas template
Home » , » TANGA RAHA- Sehemu ya Ishirini na Tano ( 25 )

TANGA RAHA- Sehemu ya Ishirini na Tano ( 25 )

Written By Bigie on Friday, March 9, 2018 | 11:41:00 AM

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA

Galfa hali ya hewa ikaanza kubadilika mbela ya madhabahu na upepo mkali ukatawala na radi vikaanza kutawalia kila pande ya madhabahu ila watu walio kuwepo wakabaki wakiwa wamesimama huku mikono yao wameinyoosha mbele kana kwamba wanapokea kitu kutoka juu.Mwanga mkali ukatoka kwenye sehemu ya madhabahu yao na gafla wakatokea watu wawili walio valia nguo nyeupa na mmoja akiwa ni mwanaume na mwingine akiwa ni Olvia Hitler na kunifanaya mwili mzima kunyong’onyea na kuishiwa nguvu kabisa

ENDELEA
    Olvia Hitler akasimama katikati ya mchungaji na muumini mwengine na akawawekea mikono kichwani mwao na kuanza kuzungumza maneno ambayo sikuwa ninayeelewa na kusababisha hali ya hewa kuzidi kutisha ndani ya kanisa lao la siri ambalo kusema kweli linatisha kupita maelezo.Upepo mkali mithili ya kimbunga ukaanza kuzunguka kwa kasi ndani ya kanisa huku kikiwa kama kinachungunza kitu fulani ndani ya chumba
 
“Eddy tuondoke ule upepo ni jini linaanalia usalama”
Tukaanza kutambaa chini mimi na Yudia na kabla hatujaufikia mlango tulio ingilia tukastukia watu wawili walio valia nguo nyeusi zilizo wafunika hadi vichwa vyao wakasimama mbele yetu.Yudia akasimama na kuwasukuma huku na yeye akiwa anazungumza manena ya ajabu kawa wafanyavyo watu waliomo ndani ya kanisa lao na kuwafanya watu hao kuangukia pembeni kisha na mimi nikanyanyuka na tukaanza kukimbia kuelekea kwenye mlango mwengine ambao ni tofauti n mlango tulio ingilia.Katika mlango tulio ingili tukakuta vipande vya miti vilivyo fungwa tambaa lenye mafuta ya taa vikiwaka huku vikiwa vimechomekwa kwenye  sehemu za ukuta wa sehemu hii na kuufaanya mwanga wake kuwa hafifu tofauti namwanga wa taa,Yudia akachomoa kimoja na kutangulia mbele huku akiniomba nimfwate
 
Tukaendelea kutembea kwa mwendo wa haraka huku kila wakati nikiwa nitazama nyuma kuangalia kama kuna watu wanao tufwata ila sikuona,Tukaendelea kwenda mbele urefu kidogo nikaanza kusikia kelele za watu wakilia na wasiwasi wangu ukaanza kunitawala
“Eddy usiogope hao ni miongoni mwa watu wanao sadikika kuwa duniani wamekufa ila wapo huku wamehifadhiwa na kila ifikapo mwisho wa wiki wawili huwa hutolewa sadaka ya kuteketeza”
 
“Sadaka ya kuteketeza ndio sadaka gani?”
“Yaani wanapelekwa mbele ya Mungu wao ambeye ni yule mzee aliye kuja na yule mwanamke ndio malkia wao”
Tukafika sehemu ambayo tukakuta chumba kikubwa chenye giza kilicho fungwa na gati kubwa huku kukiwa na mnyororo ulio fungwa na kufuli kubwa kiasi kwamba si rahisi kwa mtu kutoka ndani ya chumba hichi.Yudia akasogea huku akiwa ameshika kipande cha mti kinacho waka na kumulika kwa ndani ya chumba hicho na kujikuta nikiona watu wenye ngozi nyeusi mithili  wamepakwa vumbi la mkaa huku wakiwa na nywele ndefu na chafu kiasi kwamba kinawafanya watishe tu kwamuonekano wao wakaanza kunyoosha mikono wakiomba msaada wa kutoka huku wengi wao wakiwa ni wamama na wanaume
 
“Eddy watu hawa wanateswa sana na laiti baba na mama wakikushika nao watakuleta huku”
“Hawa hawawezi kutoka?”
“Hawawezi kwani hawa huki duniani walipo kuwa walisha zikwa na watu walisha wasahau”
Tukazidi kwenda mbele huku nikijiuliza maswali ni jinsi gani Yudia amekuwa jasiri wa kuweza kuyatambua mambo ambyao ni yakuzimu japo kwa muonekano wake ni binti mdogo sana
“Yudia umeyajuaje haya mambo?”
“Baba na mama walinichagua mimi kuwa miongoni mwa waridhi wao katika kanisa lao kishetani tangu mimi nikiwa mdogo,Kwa mara ya kwanza tulikuwa Marekani basi mama na baba wakawa wananifundisha mbinu zao zote ndio maana utaona siwaheshimu kwa maana wana roho mbaya na pele ulipo kuwa ukiona wanawekewa mikono kichwani walikuwa wanapewa nguvu na za ziada za kuweza kukukabili wewe”
“Mmmmm kwani mimi nina nguvu gani ya kuwafanya wao wapewe nguvu ya kunikabili mimi?”
 
“Eddy wewe kuna watu wanakulinda pasipo wewe mwenyewe kujua kama wanakulinda......Na watu hao ndio wanaokufanya wewe usiletwe huku na ikitokea watu hao wakauwawa basi wewe ndio utakuwa mwisho wa maisha yako kwa duniani na utaletwa huku kwenye shimo la giza na utakuwa ni miongoni mwa wale watu tulio wapiti pele wakiomba msaada”
“Yudia wale watu ulio wasukuma hawata weza  kutufwatilia?”
“Wale hawawezi kutokana nimeyapoteza mawazo yao na kwanza walikuwa wamechelewa kwenye ibada na pale wamerudi majumbani mwao na afadhali nimekutana nao mimi na kama wangekutana na baba mwenye au kiongozi yoyote mule ndani ya kanisa leo wangesimulia”
 
Tuakafika kwenye sehemu yenye vichwa vingi vya watu walio wafiki duniani na mifupa ya miili yao imezagaa kila sehemu ya chumba hichi,Yudia akaokota fuvu moja na kunipa nikishike kipande cha mti kinacho waka moto
“Hili fuvu lilikuwa la msanii mmoja maarufu Tanzania na yeye nyota yake ilikuwa ni kubwa sana ila akishindwa kuiongoza na mwisho wa siku akajikuta akiletwa huku na kutolewa sadaka”
Kila kitu anacho nieleza Yudia kikazidi kunichanganya kiasi kwamba nikajikuta nikikaa kimya pasipo  kumuuliza kitu cha aina yoyote.Tukaondoka sehemu hii na kuzidi kwenda mbele na kutokea sehemu nyenye ngazi tukapanda na kutoka nje na tukatokea kwenye moja ya bustani zilizopo kwenye jumba la mchungaji.
 
“Eddy kuna pete nitakupa ambayo hawa watu hawata weza kukuona hata yule mkuu wao kwani hii pete ninayo mimi mwenyewe tu na nilipewa kipindi nipo mdogo na mzee ambaye alikuwa ni kiongozi wao kipindi cha nyuma na alitokea kunipenda na kunifundisha mambo mengi”
Tukaingia ndani na moja kwa moja tukapanda gorofani na kabla hatujaingia chumani kwake mlango wa chumba kimoja ukafungulia na akatoka mfanyakazi wa ndani na akaonekana kustushwa sana baada ya kutuona,akataka kurudi ndani ila Yudia akamuita na kumgandamiza ukutani kama mtu anayetaka kumpiga msichana wa watu
“Nisikilize wewe OLE WAKO.....OLE WAKO NISIKIE UMEMUAMBIA MTU YOYOTE KUHUSIANA NA HILI TUKIO LA KUINGIA NA EDDY CHUMBANI KWANGU.....UTANIJUA MIMI NI NANI”
 
Msichana wa kazi akatingisha kichwa akionekana kuelewa onyo hili kisha Yudia akamuachia na msichana wa kazi akarudi ndani kwake kwa haraka kisha mimi na yeye tukaingia ndani kwa Yudia.Chumba cha Yudia kimetawaliwa na mapicha makubwa ya makatuni huku kikiwa kimepangwa vizuri kwa umaridadi wa hali ya juu na kukifanya kiwe vizuri.
Akafungua kwenye droo ya kabati lake na kutoa kisanduku kidogo cha chuma kisha akakifungua kwa namba za siri anazo zijua yeye mwenyewe na kikafunguaka na akatoa pete moja nzuri ya kung’aa sana kisha akanisogelea na kuniomba nimpe mkono wangu wa kushoto kisha akanivisha kwenye kidole cha kati na kwauzuri ikakaa vizuri
 
“Eddy ninakuomba usiivue hii pete kwa maana siku ukiivua ndio utakuwa mwisho wa maisha yako....na kama unataka kujikinga na kitu kibaya wewe inyooshe mbele na kitu hicho hakita weza kukudhuru hata wale wanao kutafuta pia hawata weza kukudhuru ikiwemo kina baba na majini wake”
Yudia akanibusu mdomoni kisha akanifungulia mlango wa chumbani kwangu na kuniomba nitoke.Nikaelekea chumbani kwangu na sikupata usingizi hadi kukapambazuka na mlango wangu ukagongwa na nikashuka kitandani na kuufungua mlango nikakutana na mama mchungaji akiwa amejifunga matenge yake akionekana ametoka kulala
 
“Eddy Bwana Yesu asifiwe”
“Amen”
“Umeamka salama?”
“Ndio mama sijui nyinyi mumeamkaje?”
“Salama tu....Chai ipo tayari karibu mezani”
“Asante mama”
Mama mwenye nyumba akaondoka na nikabaki nikimtazama kwa macho ya kujiuliza ni kwanini wanakuwa na roho za ajabu.Nikafunga mlango wangu na kuingia bafuni na kusimama mbele yak ii kikubwa kilichopo ndani ya bafu hilo,nikafungua maji kwenye bomba na kuanza kunawa uso wangu gafla nyuma yangu kukasimama mtu mwenye sura ya kutisha na kunifanya nistuske ila nikaona kama anashangaa shangaa huku akinusa nusa kwenye sehemu niliyo simama na nikagundua hanioni ndio maana ana nusa nusa.

Nikasogea pembeni taratibu pasipo kumgusa kisha nikamyooshea mkono wa kushoto wenye pete na kustukia mtu huyu akianza kuyumba huku akitokwa na damu iliyo chananyikana na uweusi mdomoni mwake na hapa ndipo nikaamini kuwa pete aliyo nipa Yudia inafanya kazi vizuri.Nikaushusha mkono wangu na kumfanya mtu huyo kupotea mbele ya macha yangu na damu zote zilizo tapakaa chini zikawa zimepotea kwenye sakafu.

Sikuogopa sana kutokana vimbwanga kama hivi nimevizoea na kwanu ni kawaida sana kuona vitu kama hivi.Nikatoka bafuni na kujifuta maji na taulo kisha nikajiweka sawa nguo zangu na kutoka ndani kwangu na kuelekea sebleni na kuwakuta watu wote wakiwa wamejumuika mezani kwa ajili ya kunywa chai,nikakaa kwenye kiti kilicho andaliwa na kusalimiana na kila mmoja na mchunajia akatuomba tufumbe macho yetu ili aongoze sala.Tukaanza kunywa chai taratibu huku mara kwa mara macho yangu yakiwatazama mchungaji na mke wake na kujikuta nikijisemea kimoyo moyo
 
“Kwa mtindo huu mbinguni kufika ni baadaye sana”
Tukamaliza kunywa chai na kuwaomba mchungaji na mke wake waniruhusu kuna sehemu ninahitaji kwenda
“Sasa Eddy huoni kama tutachelewa kufanya maombia nyumbani kwako?”
“Hiyo seemu ninayo kwenda sio mbali sana na hapa....Ninakwenda kuchukua pesa yangu mara moja kisha nitarudi”
“Ahaaa huyo mtu unamdai kiasi gani cha pesa”
“Laki nane”
“Mama Yudia nenda kwene koti langu la suti niliyo ivaa juzi kuna pesa naomba utoe laki nane na nusu uje nazo hapa”
“Lakini baba si mumuache aende zake munamng’ang’ania nini kwani ni ndugu yetu huyu?”
 
Yudia alizungumza kwa kisirani kama alivyokuwa akifanya jana usiku na kuwafanya watu kadhaa walio kaa mezani kuguna akiwemo na Junio
“Dada Yudia kwanini unamchukia sana kaka Eddy?”
“Na wewe koma sizungumzi na mbwa naongea na mwenye mbwa.....SAWA?”
“Ehhe Yudia mwanangu mbona unatabia mbaya kiasi hichi hata hupuumziki hujui kama kuna wagani au hakuana”
“Mama na wewe hizo roho zenu za ajabu ajabu zitawaponza na sitaki mumpe pesa yoyoyte”
“Mama Yudia hembu achana neye nenda kalete hizo pesa”
“Mama ukienda kuanzia leo mimi sio mtoto wenu wa kumzaa.....Hamuwezi kumpa mtu baki pesa zite,Yeye amekuwa nani hadi mumpe?”
“Mchungaji ili musigombane na Yudia ngoja mimi niende mara moja ila nitarudi muda sio mrefu”
“Basi ngoja nimuambie Joseph akaupeleke na gari”
“Hapana mchungaji nitarudi muda sio mrefu”
“Sawa”
 
Yudia akanyanyuka na kutoka nje na mimi nikaagana nao kutoka na sikumuona Yudia sehemu alipo ila sikuwa na shaka sana,Mlinzi wa gatini akanifungulia geti na kumkuta Yudia akiwa amesimama pembeni ya geti huku machozi yakiwa yanamwagika
“Yudia mbona unalia?”
“Eddy najua kwamba huto rudi tena huku na nilifanya vile ili wasielewe kitu kinacho endelea japo nimekudhalilisha ninakuomna unisamehe”
“Usijali asante kwa yale yote uliyo nifanyia kwan sinto weza kukusamehe”
“Ngoja nikupe namba yangu ya simu”
Yudia akaiandika namba yake ya simu kwenye simu yangu kisha na nikamtajia na yakwangu na akaiandika na akanikumbatia huku machozi yakimwagika kisha akiivua cheni aliyo ivaa shingoni na kunivisha
“Ho ni ukumbusho wangu kwako”
“Asante ila tutawasiliana”
Nikamuachia Yudia na kuondoka zangu huku nikimuacha Yudia akinipungia mkono na mimi nikampungia na kuongeza mwendo na kuondoka katika eneo la nyumba ya mchungaji na nikafka kwenye kituo cha waendesha pikipiki na kukodi pikipiki ikanipeleka hadi kwenye shule ninayo ifundisha na baadhi ya wanafunzi wakaja kunipokea kwa furaha.

Wakanisindikiza hadi ofisini na kuwakuta waalimu wengine nao wakaonekana kufurahi kwa kuniona japo nimewakuta wapo kwenye kikao.Wanafunzi wakarudi zao madarasani na mimi nikasalimia na waalimu wote na kukaa kwenye kiti changu nilicho kizoea na kikao kikaendelea kama kawaida na mada kubwa ilihusiana na utivu wa nidhamu kwa baahi ya waalimu wa kike.Mwalimu aliye kanywa sana ni Madam Recho ambaye amezoeleka kuwa anatabia ya uchonanishi kwa baadhi ya waalimu na hata baadhi ya wazazi wanao taka kuwahamishia watoto wao kwenye shule yetu.Sikuchangia kitu cha aina yoyote hadi kikao kikaisha.Mwalimu mkuu akaniita ofisini kwake na sikuwa na tukaongozana hadi ofisini kwake
 
“Sir Eddy unaendeleaje?”
“Salama tuu mkuu sijui nyinyi hapa?”
“Sisi tunaendelea salama”
“Vipi Zena Alisha toka hospitali?”
“Ndio aliruhusiwa jana yupo nyumbani kwake kama utapata muda tunaweza kwenda kumuona”
“Sawa”
Kabla mkuu wa shule hajazungumza chochote mlango wa ofisini kwake ulagongwa na akamruhusu anaye gonga kuingia.Akaingia rafiki wa Rahma na kumuomba mkuu wa shule boksi za chaki ambazo ameagizwa na mwalimu wa taaluma.Akaonyeshwa boksi kubwa lenye chaki analibeba na kuondoka nalo na kumfanya mkuu wa shuke kubaki akimtazama rafiki wa Rahma kwa nyuma jinsi makali yake yanavyo tingishika
“Mmmm watoto wa siku hizi”
“Wana nini mkuu?”
“Wanadatisha sana mtu unaweza ukajikuta unafungwa hivi hivi”
 
“Haaa ndio hivyo mkuu”
“Ila kuna mtoto wa kiarabu ninamfukuzia hadi leo ila bado hajanikubalia”
“Kwa nini hajakukubalia?”
“Mtoto kila nikimpa maneno matamu ya kiutu uzima anadia kuwa atanijibu na tayari ameshanilia pesa yangu si chini ya milioni”
“Ehee”
“Kweli Eddy ninakuambia hivi kama mwanangu na hapa shule nataka nifanye mapinduzi kidogo ya utawala....”
“Kwa nini?”
“Nimeamua tuu nataka nifanye mpango wa kukupandisha wewe na kuwa makamu mkuu wa shule”
“Huyu wa sasa hivi naye atakuwa wapi?”
“Huyu anahama zimebaki siku tatu za yeye kuwepo hapa na mimi kama mkuu wa shule ninahitaji kupendekeza mtu mwenye akili timamu.....Sio kama hawa kina Recho akili zao zipo makalioni hawaheshimu kazi kabisa”
 
“Mkuu huoni majukumu unayo nikabidhi nimakubwa tofauti sana na muda wangu nilio kuwepo kazini?”
“Ahaa muda wako wa kuwepo kazini hauna shida cha msingi ni utendaji wako wa kazi kuna watu wapo kazini sasa ni mwaka wa 30 ila utendaji wao ni mbovu kupindukia”
“Sasa itakuwaje kwa waalimu wanao nichukia?”
“Wewe unaogopa kuchukiwa potelea pote ila cha msingi ni kwamba unakuwa msaidizi wangu ila kuna kajikazi nahitaji nikupe kwa maana wewe unapendwa sana hapa shule na wanafunzi wengi hilo halipingiki”
“Kazi gani mkuu?”
“Nahitaji unifanyie mpango kwa yule msichana niliye kuambia”
“Anaitwa nani?”
“Anaitwa RAHMA anasoma kidato cha nne”
Nikajikuta nimekaa kimya nikimtazama mkuu wa shule huku nikijiuliza kama akili zake zinafanya kazi sawa sawa au ndio uzee unamchanganya

  ITAENDELEA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya