0657072588
ILIPOISHIA
Katika chumba hichi kikubwa, kina chumba kingine ndani cha kulala, na hapa tulipo simama ni sebleni.
“Dany ninakuomba”
Olvia Hitler alizungumza huku akiingia ndani ya chumba cha kulala, nikamfwata kwa nyuma huku tukimuacha Vivian akiwa amekaa kwenye moja ya sofa kubwa lililopo kwenye hichi chumba. Olvia Hitler akachukua rimoti na kuwasha Tv, kisha akanigeukia na kunitazama machoni mwangu.
“Upo tayari kumfahamu mtu anaye miliki lile gereza?”
“Ndio”
“Huto kasirika?”
“Mmmmm wewe niambie tu”
Olvia akakaa kimya kwa muda huku akionekana akitafakari kitu cha kuzungumza na kunifanya nizidi kuwa na hamu ya kuhitaji kumfahamu mmiliki wa gereza ni nani.
ENDELEA
“Hakuna haja ya kukuambia sasa, utafahamu”
“Ile umeniahidi kuniambia”
“Ndio nimekuahidi, ila muda na wakati utakapo fika unaweza kufahamu”
Olvia Hitler alizungumza huku akitoka chumbani, sikuhitaji kumsemesha chochote kwa maana mimi na yeye tuna utofauti mkubwa sana kwenye huu ulimwengu. Kitu ambacho kinaniumiza kichwa ni kwa nini Olvia Hitler anaishi maisha ambayo si rahisi kwa mtu kuweza kumfahamu kwamba yeye ni jini.
Nikatoka chumbani na kumkuta Olvia Hitler akimalizia kuzungumza na simu, sikujua anazungumza na nani.
“Dany nimeagiza chakula, sasa sijafahamu ni chakula gani ambacho unakipendelea?”
“Chochote”
“Basi hakuna shida. Kesho asubuhi nitakwenda kuwatafutia hati za kusafiria, ili muweze kurudi Tanzani”
“Wewe je hurudi?”
“Mimi kuna mambo nahitaji kuyamalizia”
“Sawa”
Haukupita muda mrefu chakula kikaletwa na muhudu, taratibu tukaanza kula kwa pamoja, ila muda wote Vivian yupo kimya hazungumzi jambo la aina yoyote. Uso wake unaonekana ni mtu ambaye amejawa na wingi wa mawazo.
“Vivi una tatizo gani?”
“Mmmm”
“Ila unaonekana kama umejawa na mawazo?”
“Hapana sina kitu”
Vivian alizungumza kwa ufupi, sikuona haja ya mimi kuendelea kumuhoji maswali mengi. Tukamaliza kula, kutona bado ni usiku na tumepitia ngija ngija nyingi nikaona si vibaya nikajipumzisha kwenye kochi na kuwaacha Olvia Hitler na Vivian wazidi kuzungumza mambo yao. Usingizi mzito ulio jaa njonzi zuri, ukaendelea kunibeleza taratibu, huku masaa yakienda taratibu.
“Dany amka”
Niliisikia sauti ya Vivian karibu yangu, taratibu nikafumbua macho, nikamuona akiwa amekaa pembeni ya sofa. Akanitazama usoni mwangu. Nikajinyanyua, nikatazama kila mahali mwa hii seble ila sijamuona Olvia Hitler.
“Vipi yupo wapi Olvia?”
“Amekwenda kutafuta hizo hati za kusafiri.”
“Aahaha sawa sawa”
“Alafu Dany kuna kitu ninahitaji kukuuliza japo ninaogopa?”
“Kitu gani?”
Vivian akaka kimya huku akipnekana kukiwazia hicho ambacho ahahitaji kuniuliza. Akayananyua macho yake na kunitazama usoni mwangu kwa haraka kisha akayanshusha chini alipo kuwa anapatazama kwa mara ya kwanza.
“Nini?”
“Ahaa basi”
“Zungumza”
“Hivi huyu Olvia mimi mbona simuelewi elewi?”
“Umuelewi elewi kivipi?”
“Ananiogopesa sana, nahisi kama si…….”
Vivian hakumalizia sentensi yake mlango wa sebleni ukafunguliwa na akaingia Olvia Hitler akiwa amevalia koti jeusi pamoja na suruali nyeusi na mkononi mwake amevaa gloves za kuzuia baridi kali inayo endelea huko nje.
“Dany umeamkaje?”
“Salama”
“Ninahabari nzuri, nimefanikiwa kupata hati za kusafiria. Pia nimefanikiwa kupata ndege itakayo ondoka saa sita kamili machana”
Olvia Hitler alizungumza huku akitukabidhi kila mtu hati yake ya kusafiria. Nikaichukua ya kwangu na kuifungua ndani, macho yangu yakakutana na sura yangu kwenye picha ndogo pembeni na majina yangu kamili. Sikuhitaji kuuliza swali kama Olvia Hitler hizo picha amezipatia wapi kwa maana ninautambua uwezo wake wa kijini ambao amepewa. Vivian akaonekana kama mtu mwenye maswali ila akajitahidi kulizuia swali lake. Uzuri ninafahamu jinsi ya kumsoma mtu mwengine kwa haraka sana na kuweza kufahamu anacho kiwaza ni nini kwa wakati huo, kwani uwezo huu ni moja ya mafunzo niliyo yapata darasani kipindi nikijifunza maswala ya usalama wa Taifa.
“Shukrani sana, sasa tutasafiri na hizi nguo za jeshi?”
“Hapana, hizo nguo mutazibadilisha, kitu cha muhimu kwa hivi sasa, ni kuanza kujiandaa”
“Asante eheee”
Vivian alizungumza huku akimtazama Olvia Hitler kwa macho ya kuibia ibia. Kifungua kinywa kikaletwa chumbani na muhudumu, mimi na Vivian ndio tukanywa hichi kifungua kinywa.
“Sijui nikawaletee nguo ili tuokoe muda?”
“Itakuwa vizuri”
“Sawa”
Olvia Hitler akaondoka na kutuacha mimi na Vivian ambaye baada ya mlango kufungwa, akanisogelea karini kabisa na sehemu nilipo kaa.
“Dany hivi huyu dada wewe uhisi utofauti wowote?”
“Utofauti gani?”
“Huwa akiwa humu ndani, damu yangu inasisimka, kitu ambacho si jambo la kawaida kwa mwadamu, kusisimka katika hali ya utulivu.”
Vivian alizungumza kwa sauti ya chini. Nikatamani kumueleza ukweli kuhusiana na Olvia Hitler, ila mdomo ukasita kabisa kuzungumza jambo kama hilo kwa maana sifahamu ni kitu gani ambacho kinaweza kwenda kutokea baada ya kuzungumza jambo kama hilo.
“Ahaa itakuwa labda ni mwili wako au damu zenu haziendani. Mbona mimi ninazungumza naye na ninaona ni wakawaida sana”
“Hivi ukimshika auhisi ubaridi fulani kwenye mwili wake?”
“Hapana sihisi chochote”
“Mmmm labda ni mimi mwenyewe”
“Yaaa”
Sikuhitaji kuendelea na mazungumzo hayo, nikanyanyuka na kuelekea chumbani ambapo kuna bafu, nikaoga kwa ajili ya kujiandaa. Baada ya kumaliza na kurudi sebeleni nikamkuta Olvia Hitler akijaribisha Vivian nguo alizo mnunulia na wote wanaoenekana wapo kwenye furaha sana.
“Dany nimepata nguo zako hizo hapo kwenye mfuko”
“Shukrani”
Nikachukua nguo zangu na kurudi nazo chumbani, nikazivaa. Kusema kweli zimenibadilisha sana, tofauti na jinsi nilivyo kuwa gerezani. Japo ni siku chache tangu niingie kwenye lile gereza ila, nilichakaa sana kutokana na mateso ambayo nilikuwa ninayapata mara kwa mara.
Baada ya Vivian kumaliza kujiandaa, safari ya kuelekea uwanja wa ndege ikaanza huku Olvia Hitler akiwa anaendesha gari na kila mtu alitupatia dola elfu tano zitakazo tusaidia mbele ya safari. Tukafika uwanja wa ndege, Olvia Hitler akanivuta pembeni ili kuzungumza na mimi.
“Nakutakia maisha mema huko huendapo, ila kumbuka kwamba kwa sasa nina kiumbe tumboni mwangu, na atazaliwa baada ya muda mchache nikurudi chini ya bbahari”
“Ukirudi chini ya bahari?”
“Ndio, kule ndio nyumbani kwetu”
“Mmmmm”
“Yaaa usishangae sana, hichi kiumbe atakusaidia sana kwenye maisha yako yajayo”
“Atakuwa binadamu?”
“Yaaa atakuwa binadamu ila atakuwa na nguvu tofauti na binadamu, mimi niwatakie safari njema na nitaendelea kuwa karibu nanyi huko muendapo”
“Sawa shukrani”
Baada ya kumaliza mazungumzo hayo, tukarudi sehemu alipo kaa Vivian. Akaagana naye ila kabla ya kuondoka ikabidi nimshike mkono Olvia Hitler na kuzungumza naye pembeni.
“Samahani mpenzi”
“Bila samahani?”
“Mimi Tanzania ni ninatafutwa sana, sasa utanisaidiaje katika hilo?
“Usijali, nitakulinda”
Olvia Hitler alizungumza huku akitabasamu. Akaondoka na kutuacha mimi na Vivian tukiwa tumesimama tunamtazama anavyo jichanganya na watu wanaotoka kwenye uwanja huu wa ndege. Tukaanza kufwata taratibu zote ambazo abiria wanao safiri wanatakiwa kuzifwata. Sehemu zote za ukaguzi tukapita salama na kuelekea eneo la kuingilai kwenye ndege. Tukaingia kwenye ndege shirika la Fast Jet, Tukakaa kwenye siti ambazo zina namba kutokana na tiketi tulizo nazo.
Uzuri wa siti zetu zipo kwa pamoja, tukafunga mikanda yetu, haukupita muda mrefu sana safari ikaanza taratibu huku ndege ikiwa imejaa abiria wenye asili tofauti tofauti. Furaha ikanijaa moyoni mwangu, kwa maana ninakwenda kuiona familia yangu. Ila swala la Olvia Hitler kuhitaji mtoto kutoka kwangu likaendelea kutawala kwenye mfumo wangu wa mawazo.
“Dany mbona una mawazo?”
“Ahaa ninakumbuka mambo mengi sana kuhusiana na nyumbani Tanzania”
“Wewe una nafuu, kwa maana mimi nina miaka mingi tangu nilivyo tekwa na kupelekwa kwenye mafunzo kwenye moja ya meli kubwa jamboa ambalo lilinifanya niishi kigaidi na niishi kama jike dume”
“Ngoja kwanza umezungumzia swala la kwenda kufanya mazoezi kwenye meli kubwa?”
“Ndio kwani unalifahamu hilo swala”
“Ahaaa nilisha wahi kulisikia, na pia kuna binti mmoja naye alikuwa anafanya mazoezi katika hiyo meli”
“Anaitwa nani?”
“Mariam”
Sura ya Vivian ikabadilika, huzuni ikaanza kumtawala kwenye sura yake. Wasiwasi mwingi ukaanza kuniingia.
“Unamfahamu?”
“Yaa, alikuwa ni rafiki yangu mkubwa sana mafunzoni, japo alinikuta kwenye yale mafunzo”
Vivian alizungumza kwa sauti iliyo jaa huzuni.
“Nilipo kuwa gerezani nilionyeshwa video yake akiteseka, na kutokana na video yake niliambiwa kwamba nipigane kwenye yale mashindano ya kuuana”
“Bora pia hujapigana, ila ukweli ni kwamba Mariam hivi sasa ni MAREHEMU”
Maneno ya Vivian uakawa kama yameupiga moyo wangu konde zito ambalo nimeshindwa kulihimili na machozi taratibu yakaanza kunitiririka kwa maana ninamfahamu Mariam kwa muda mrefu sasa.
“Ila kuna watu ambao ninawajua walio pelekea kifo cha Mariam, tukifika Tanzania tutahakikisha kwamba tunamsaka mmoja baada ya mwengine na wote tunawaangamiza”
“Unawajua?”
“Ndio ninawafahamu, na picha zao nimezihifadhi kwenye email yangu”
Vivian alizungumza kwa kujiamini sana, taratibu nikajifuta nikiyafuta machozi yangu huku nikitamani sana kuweza kuwajua watu walio pelekea kifo cha Mariam. Tukiwa katika ndege kwa kupitia dirishani nikaona hali ya mawingu ikibadilika, mwanga ukamwezwa na wingu zito la mvua, ambalo lina rangi ya kijivu. Sikulitilia maanani kwa maana ni jambo la kawaida katika hali za hewa. Kadri tunavyo zidi kwenda mbele ndivyo jinsi hali ya hewa ilivyo zidi kubadilika hadi ikafika hatua zikaanza kupiga radi nyingi na zenye miyanga mikali sana.
“Mmmm”
Vivian alighuna tuu baada ya mwanga mkali kuonekana kwenye dirisha la pembeni yangu.
“Samahani kaka unaweza kufunga dirisha”
Muhudumu alizungumza, huku akinitazama, nikashusha kijipazia kidogo ambacho kinanifanya nishindwe kuaona kitu kinacho endelea nje. Hazikupita hata dakika mbili, tukasikia mtikisiko mzito kwenye ndege na kutufanya abiria wote kuhamaki.
“Abiria tunaomba mufunge mikanda yenu”
Tuliisikia sauti ikitokea kwenye kipaza sauti. Walio ifungua mikanda yao wakaanza kufanya hivyo, hata Vivian naye akafanya hivyo, ukatokea mtikisiko wa pili ulio tufanya abiria kuanza kusali sala wanazo zifahamu wao. Gafla taa zote zikazimika, ndege ikaanza kuyumba na kupelekea mizigo iliyo wekwa sehemu maalumu kuanza kuanguka hovyo hovyo, hapo ndipo nilipo anza kusikia vilio vya wamama na watoto wakilia huku wakiliita jina la Mungu aliye umba mbingu na ardhi.
AISIIIII……….U KILL ME 82
Hali ndani ya ndege ikazidi kuwa mbaya baada ya ndege kuanza kuzunguka kwa kasi sana. Mabegi yakendelea kutuangukia. Kusema kweli wewe sikia tu kwamba kuna ajali za ndege ila usitamani kuwa ni mmoja kati ya watu wanao kumbwa na janga hili la kutisha sana. Sikumuona wala kumsikia Vivian aliye kuwa amekaa pembeni yangu kwa maana hata siti za ndege hii zimeanza kung’oka na kupeleka hali hii kuwa mbaya zaidi.
“Mungu nisamehe zambi zangu nilizo zifanya.”
Nilizungumza maneno hayo baada ya kuona kipande cha ndege kimeguka na kuufanya upepo mwingi kuingia ndani ya ndege, na kuanza kuwatoa watu wengine ambao viti vyao vimeng’oka. Kitu ambacho nimekisikia ni mivunjiko ya matawi ya miti, nikajikuta nikijigonga kichwa changu kwenye moja ya kitu kizito na hapo giza zito likatawala mfumo wangu wa kuona na nikatulia kimya.
***
Milio ya risasi nikaanza kuisikia kwa mbali sana kwenye masikio yangu. Milio hii inayo sikika kwa kupokezana, ikanifanya nijitahidi sana kuyafumbua macho yangu. Nikafanikiwa kufumbua jicho la upande wa kushoto, ila jicho la upende wa kulia limejawa na giza zito. Nikayachunguza mazingira ya eneo hili nililopo, mwanga unao ingia kwenye kijidirisha kidogo, ukanisaidia kuona vitu vichache katika chumba hichi ikiwemo, kijikitanda kidogo ambacho nimelalia. Pembeni ya hichi kitanda kuna kijikiti kidogo cha chuma.
Nikajitazama miguuni mwangu, nikaona mguu wa kushoto ukiwa umefungwa bandeji kubwa sana, hadi maeneno ya pajani. Taratibu nikajigusa jichoni mwangu, napo nikakutana na bandeji zito likiwa limezunguka kichwa changu kizima na sehemu ambayo ina uwazi ni masikio, jicho moja, mdomo pamoja na pua. Mikono yangu nikaitazama, nikaikuta na makovu mengi yaliyo pakwa pakwa dawa.
Nikajikuta nikishusha pumzi nyingi, huku nikitazama dari la chumba hichi ambalo limesindikwa na udogo mwingi. Kumbukumbu za ajali zikaanza kujirudia tena kichwani mwangu, kitendo cha kumbukumbu kunijia kichwani mwangu, kinanifanya kichwa changu kuniuma sana.
Akaingia binti aliye valia baibui, lililo ficha sura yake na kubakisha macho yake. Mikononi mwake ameshika kikombe chenye kijiko. Alipo ona ninamtazama, akasimama kwa muda akataka kutoka, ila akanisogelea na kukaa kwenye kijikiti hichi cha chuma. Akakoroga kitu kilichopo kwenye kikombe hichi, kisha akachota kidogo kwenye kikombe na kunisogezea mdomoni majimaji haya yenye rangi ya kijani.
Nikafumbua mdomo wangu taratibu na kuyapokea maji haya ambayo, kitendo cha majimaji haya kugusana na ulimi wangu, nikahisi uchungu ambao tangu kuzaliwa kwangu sikuwahi kuupata. Nikashindwa kabisa kuyameza majimaji haya na kujikuta nikitatema pambeni.
Msichana huyu akanitazama kwa macho makali kidogo, kisha akarudia kuchota dawa hiyo kwa kijiko na kunisogezea mdomoni mwangu. Nikajifikia kidogo, kisha nikaipokea kijiko hicho kwa kufumbua mdomo wangu. Uchungu wa hii dawa, kusema kweli imezidi hata uchungu wa dawa moja inayo itwa Cloroquin. Nikaendelea kujikaza kunywa vijiko hivyo vya dawa hadi kikombe kikaisha kabisa. Msichana kwa kupitai macho yake nikaona akiwa amejawa na furaha. Akanyanyuka kwenye kiti alicho kalia, na kutoka ndani ya chumba hichi. Kitu kinacho nishangaza ni jinsi milio ya risasi inavyo endelea nje ya chumba hichi na wala msichana huyu aliye toka wala hakuonekana kuonyesha kwamba ana wasiwasi wowote katika hilo.
Baada ya lisaa milio hiyo ya risasi ikanayamaza, nikiwa katika kuendelea kusikilizia kama hiyo milio itaendelea tena. Mlango wa chumba hichi kikafunguliwa na akaingia Mzee mmoja mwenye ndevu nyingi kwenye kidevu chake pamoja na msichana ambaye aliniletea dawa, japo sijaiona sura yake ila kifua chake kilicho fungasha chuchu zilizo chongoka, zikanifanya nitambue kwamba huyu ni msichana.
“Asalam alyakum”
Mzee huyu alizungumza huku akikaa kwenye kijjiti hichi cha chuma na msichana huyu akasimama pembeni ya mzee huyo.
“Salama”
Nikawajibu kwa kiswahili, mzee huyu akatazamana na msichana huyu kisha wakanitazama tena kwa nyuso zilizo jaa furaha.
“Naitwa General Ahamad Suleima. Huyu ni binti yangu anaitwa Hawa Ahamad Suleima, sijui wewe mwenzetu unaitwa nani?”
“Naitwa Dany”
“Karibu Somalia”
“Eheee!!”
Nilishangaa huku nikimtazama General Ahamad kwa jicho langu hili moja.
“Usishange sana, binti yangu alikuokota huko porini kwenye ajali ya ndege, hali yako iliuwa ni mbaya sana, ila Mwenyezi Mungu, amesaidia hadi sasa umeamka”
Mzee huyu alizungumza kiswahili chenye lafuzi ya Kikenyaa kwa mbali japo anajaribu kunyoosha maelezo yake kwa ufasaha.
“Umekuwa nasi kwa wiki ya pili sasa tangu kuletwa kwako, Binti yangu amekuwa akikuhudumia kwa kipindi chote hicho”
Nikamtazama binti huyu ambaye muda wote ananitazama usoni mwangu.
“Asante dada”
“Karibu sana”
“Umetokea nchi gani?”
Nikaka kimya kwa muda ili kujaribu kufikiria jibu ambalo nitalitoa lisije likaniletea matatizo ambayo kusema kweli yanaweza kunipelekea kifo changu.
“Kenya”
“Ohoooo Kenya na sisi pia tuna makazi”
Mzee Ahamad alizungumza kwa furaha sana, huku akinitazama usoni mwangu.
“Hawa, mletee chakula Dany, naamini hapo utumbo unamchemka sana”
Hawa akatoka kwenye chumba hichi na mimi nikabaki na mzee huyu, ambaye kwa haraka haraka ukimtazama utatambua kwamba ni gaidi, japo usoni mwake ana tabasamu la kumshawishi mtu na kuficha makucha yake.
“Dany mwenyezi Mungu atakusaidia na utakuwa sawa”
“Amen”
“Kikubwa ni kula ili afya yako irudi, dokta ametuambia kwamba jicho lako limepata itilafu kidogo ila baada ya muda litarudi katika hali yake ya kawida, hata huo mguu wako wa utapona”
“Asante sana kwa kunisaidia mzee wangu”
“Wala usijali hilo kabisa. Mimi kwako sasa ni sawa na baba, nitakuangalia vizuri na kukutunza”
“Nashukuru sana kwa hili Mungu atakubariki”
Nikajitia na mimi kumuunga mkono kwa maswala yake, ila tayari nimesha jua ni kitu gani kinacho endelea, kwa maana nchi hii ya Somalia kila mtu anajua kwamba ni makazi ya vikundi vikundi vingi ya ugaidi huku vikiongozwa na kundi la Al-Shabab, ambalo kwa mara kadhaa limekuwa likifanya matukio ya kutisha nchini mwake na hata nje ya nchi yake.
Hawa akaingia huku akiwa ameshika sahani yanye wali pamoja na maharage juu yake. Baba yake akampisha kwenye kiti alicho kuwa amekaa. Hawa taratibu akaanza kunilisha chakula hichi, ambacho nina muda mrefu sijakila. Tumbo ni kweli lina njaa kali kwa maana hata kijiko ambacho ninapewa, ninakitafuna kwa haraka haraka kisha ninakimeza na kupokea kingine. Kasi ya kutafuna ikaanza kupungua taratibu baada ya kuhisi tumbo langu kuanza kushiba.
“Kula kula Dany, unatakiwa kupata nguvu”
Mzee Ahamad alizungumza kwa furaha sana, huku akinitazama usoni mwangu. Nikajitahid kula hadi nikamaliza sahani hii iliyokuwa imejazwa ubwabwa.
“Sasa hapa ukimpatia na maji basi mambo yatakuwa vizuri sana”
“Sawa baba”
Hawa akanyanyuka kwenye kiti hichi na mzee Ahamad akakaa kwenye kiti hicho.
“Nakumbuka nilipo kuwa kijana kama wewe nilipataga ajali kama hiyo yako. Sema ya kwangu ilikuwa mbaya sana. Miguu yote ilifunnyika, mbavu zangu za upande wa kulia nazo baadhi zilivunjika. Yaani kila nikiikumbuka ile ajali huwa nahuzunika sana”
“Kwa nini?”
“Nilimpoteza mama Hawa, na ndio kwanza hawa alikuwa ana miezi sita. Cha kumshukuru Mungu hawa hakupata jeraha lolote wala hakuumia popote, yaani daaa”
Mzee Ahamad alizungumza huku machozi yakimlenga lenga, akajifuta machozi kwa kiganja cha mkono wake wa kulia baada ya Hawa kuingia ndani ya hichi chumba akiwa ameshika kikombe na jagi. Hawa akamimina maji kwenye kikombe na kunikalisha vizuri kitandania na kuanza kuninywesha maji haya.
Nikagugumia vikombe viwili vya maji, hapo ndipo nilipo hisi tumbo kuvimbiwa na kuhisi haja kubwa kwa mbali.
Siku zikazidi kwenda mbele, hali yangu kusema kweli ninamshukuru Mungu, kwa dawa anazo nipatia Hawa kila asubuhi, dawa zake zinaijenga misuli yangu, kwani hata mguu wangu ukaanza kupata nguvu. Japo dawa zake ni chungu sana ila zinanisaidia kwa kiwango kikubwa. Ila katika siku zote ambazo Hawa ananiletea dawa, chakula na maji. Sijawahi kuiona sura yake kabisa, amekubwa ni mtu wa kuificha sura yake.
“Itabidi leo unze mazoezi ya kutoka nje”
“Sawa”
“Ngoja nikakuletee magongo”
Hawa alizungumza huku akinyanyuka kwenye kiti, kidogo nikapata fursa ya kumtazama kwa nyuma. Japo amevaa baibui refu hadi chini, ila maeneo ya makalio amebahatika kupewa mzigo wa wastani. Akafunga mlango pasipo kufahamu kwamba nimemchunguza. Baada ya dakika tano, akarudi akiwa ameshika magongo ambayo hutumia kutembelea watu ambao wana matatizo ya miguu.
Taratibu nikajikaza kunyanyuka kitandani peke yangu na nikafanikiwa. Akanipatia magongo yote mawili nikayashika na makwapa yangu yakapita kwa juu yake, nikapata muhumili wa kusimama kisawasawa pasipo msaada wa Hawa.
Hawa akasimama pembeni yangu na taratibu tukaanza kutembea kuelekea nje, huku nikiwa makini kwa kila hatua ninayo piga. Tukatoka nje ya nyumba hii. Sikuamini wingi wa watu ninao waona mbele yangu wakiwa katika mafunzo ya kijeshi. Hii ni ngome kubwa na kuna ulinzi wa kila manma. Kitu kilicho zidi kunishangaza, ni kuwaona vijana wadogo nao wakiwa ni miongoni mwa wanajeshi katika hii ngome. Bendera yao yenye rangi nyeusi na iliyo andikwa maneno kwa lugha ya kiarabu, nikafahamu kabisa hawa ni Al-Shabab, tena nipo kwenye makao yao makuu.
“Twende huku”
Hawa alizungumza huku akinishika mguu, tukaendelea kutembea kwa utaratibu, huku baadhi ya wanajeshi ambao hawapo kwenye mazoezi, wananitazama sana. Hawa akaendelea kunionyesha baadhi ya maeneo yah ii ngome yao iligo zungushiwa ukuta mmoja mrefu kwenda juu.
“Hii yote ni ngome ya baba yangu, na yeye ndio anamiliki wanajeshi hawa wote”
“Unataka kuniambia baba anamiliki haya yote?”
Nilijifanya mjinga kuuliza uliza maswali kwa maana ninahofia kujulikana kama nilikuwa ni mpelelezi wa serikali ya Tanzania.
“Ndio anamiliki kila kitu, hili ni kundi kubwa sana ambalo baba analimiliki. Wapo wanajeshi zaidi ya laki moja, seme wengine wapo kwenye kambi nyingine kubwa maili kumi kutoka hapa tulipo.”
“Ahaa baba kusema kweli amejitahidi”
Nikiwa katika kuwatazama tazama wanajeshi hawa wa kisomali, nikamuona kijana mmoja ambaye naye amenikazia macho. Kumbukumbu yangu ikarudi hadi siku ambayo tulikuwa Tanga na raisi, na njiani tukakutana na magari ya wasomali, na tukapambana nao na kuwaua wote. Mmoja wa vijana ambao nilipambana nao ni huyu anaye nitazama sana. Kijana huyu akasimama huku bunduki yake akiwa ameishika vizuri, akaanza kupiga hatua huku akinifwata akionekana kuwa na jazba kubwa usoni mwake. Nikatamani kufanya kitu ila uwezo sina, na kitu kingine ninaogopa sana hawa watu wakifahamu kwamba mimi nilikuwa mpelelezi nchini Tanzania na nimiongoni mwa watu nilio sababisha vifo vya ndugu zao wengi sana jambo ambalo nahisi hadi leo wameweka uhasama mkubwa na nchi ya Tanzania.
ITAENDELEA
Post your Comment