Get the latest updates from us for free

mas template
Home » , » AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 87 na 88 )

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 87 na 88 )

Written By Bigie on Tuesday, April 17, 2018 | 5:05:00 PM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA                       
ILIPOISHIA   
Delifina alizungumza huku akisimama, nikatazama kwa mbali nikaona uwanja  wenye nyasi nzuri na kwa mbele kuna majengo yanayo waka taa.
“Hapa ndio ikulu?”   
“Ndio”
“Ni watu gani ambayo wanahitaji kukua?”
“Ni adui wa baba yangu, anaitwa Livna Livba na hii sio mara yake ya kwanza kuhitaji kuniua. Asante sana Dany na Mungu akubariki”
Delfina alizungumza akanibusu shavuni na kuondoka huku akikimbia. Taswira ya Livna amsaliti wangu ikaanza kunijia kichwani mwangu, nikajikuta nikitawaliwa na hasira kali na kwa haraka nikageuka na kuanza kurudi msituni huku nikikimbia, nikihitaji kumkamata mmoja wa watu wake nimpatie meseji atakayo ipeleka kwa bosi wake

ENDELEA
Ndani ya msitu mzima kazi yangu ni kuhakikisha kwamba ninawapata watu wa Livna Livba. Ila kadri nilivyo zidi kusonga mbele sikuweza kuona dalili yoyote ya mtu ndani ya huu msitu na nikajikuta nikitokea sehemu ya maegosho ya magari. Japo polisi na waandhishi wa habari walisha jitokeza kuchukua matukio ambayo yametokea katika hili eneo. Nikajipenyeza penyeza kwa watu ambao wamekusanyika pemebi wakitazama jinsi polisi wakifanya uchunguzi wao. Nikaanza kurudi kuelekea sehemu ambapo tulitokea kutoka kwenye ngome yetu ya Al-Shabab. Nikafanikiwa kufika salama pasipo mtu yoyote kuniona, nikawakuta Ruben na rafi yetu ambaye tulitoroka naye.
 
“Dany ulikuwa wapi?”
“Babu pale lile tukio lilivyo tokea, nilijibanza kwenye moja ya kona ndio muda huuu ndio ninatoka baada ya kuona mambo kutulia”
“Ahaa ilikuwa bado nusu tuingie kwa maana tulihisi ni miongoni mwa watu walio kufa”
“Ahaaa sifi  kirahisi namna hiyo”
Sikutaka marafiki zangu kuweza kufahamu kwamba kuna jambo gani ambalo nimelifanya. Tukaingia kwenye shimo letu, tukachukua tochi zetu, tukaziwasha na kuelekee sehemu ambayo inatokezea katika chumba kilichopo ndani ya ngome hii. Hatukuchukua muda sana tukafika kwenye shimo letu, akapanda mmoja mmoja. Tukafunika sehemu hii tunayo tokelezea, chumba tukakipanga vizuri, nikabadilisha nguo zangu na kuvaa nguo nilizo kuwa nimezivaa. 
 
“Sasa waskaji?”
“Poa bwana Dany japo mambo yameharibika”
“Musijali, mukipata nafasi nyingine kama hii musisahau kunialika”
“Usijali kaka, sisi kila weakend tunatoka”
“Poa poa”
Nikafungua mlango na kutoka kaatika chumba hichi. Japo ni majira ya usiku sana ila nikajitahidi kutembea kwa kujiamini kama nipo kwenye lindo. Nikafanikiwa kufika chumbani kwangu, nikaingia, nikawasha taa kuangalia  kama usalama wa chumba kipo, kisha nikaizima na kulala kitandani. Sura ya Livna Livba kwa mara kadhaa ikaanza kunitawala kichwani mwangu, kila muda ninajaribu kufikiria ni jinsi gani ninavyo weza kumpata.
 
‘Au  atakuwepo hapa Somalia?’
Nilijiuliza maswali mengi. Matumaini yakaanza kunijaa moyoni mwangu kwa maana tayari nimesha gundua njia ambayo inaweza kunisaidia kutoka katika hii kambi pasipo watu wengine kunistukia, kumshuhulikia Livna Livba kisha nitafwatia na K2 hawa ndio wanawake ambao ni maadui zangu wakubwa chini ya hili juu. Hadi kuna pambazuka kichwa changu kimesha panga mipango ya kipelelezi ya chini chini, kuhakikisha ninampata adui yangu mmoja baada ya mwengine.
 
“Ni muda wangu sasa”
Nilizungumza huku nikijinyoosha viungo vyangu, nikaanza kufanya mazoezi madogo madogo ndani ya chumba changu. Nilipo hakikisha nipo vizuri, ndio nikatoke nje kuelekea kwenye mazoezi ya kikundi.
“Jana usiku ulikuwa wapi?”
Mwalimu wangu wa mazoezi aliniuliza kwa sauti ya chini sana pasipo mwajeshi mwengine kusikia. Kidogo nikastuka ila akili yangu sasa hivi nimesha iweka katika hali ya kuweza kupanga na kupangua matatizo kwa ustadi wa hali ya juu.
“Nilikuwa kwa Ruben”
 
“Ohoo baada ya sherehe nilikuja chumbani kwako ila sikukuta”
“Yaa jana sikumaliza sherehe, nikaona nikapige pige stori na waskaji”
“Sawa sawa, jiandae kwa mazoezi”
Mwalimu wangu alizungumza na kunifanya nianze kujitayarisha kwa maozezi ya leo. Mazoezi yakaendelea kama kawaida, huku kila mwanajeshi akihakikisha anajitahidi kwa kadri anavyo weza yeye mwenyewe, ila mwalimu wangu kwa mara kadhaa mananitupia macho. Taratibu nikaanza kuhisi kuna kitu ambacho amekigundua kutoka kwangu na kitu chenyewe ni juu ya uwezo wangu. Siku zote nilikuwa mtu wa kuigiza kama mjinga ila watu walio nivamia bafuni ndio wana mfanya mwalimu wangu kunihisi, anavyo nihisi. Kwa uzuri huwa ninauweo wa kuyasoma mawazo ya mtu kuliko jinsi hata yeye anavyo hisi.
‘Potelea pote, nikimaliza kazi yangu, ninarudi Tanzania kwa ajili ya K2’
Nilizungumza kimoyo moyo huku nikiendelea kufanya mazoezi kwa juhudi sana. 
 
“Dany unaitwa”
Mwajeshi mwengine alikuja kunipa taarifa hiyo. Mwalimu akaniruhusu kwa ishara. Nikaacha ninacho kifanya na nikaanza kuongozana na mwanajeshi aliye kuja kuniita hadi kwenye ofisi ya Hawa ambaye ndio mkuu wa jeshi, amekaimu nafasi hii kutokana na baba yake hayupo.
“Unaweza kwenda”
Hawa alimuambia mwanjeshi aliye nileta hapa ofisini kwake. Hawa akaniomba nikae kwenye kiti kilichopo mbele ya ofisi yake. Nikaka huku tukitazama kwenye.
“Kuna kazi ambayo imekuja kwa muda huu, nimezungumza na baba, akakubali niifanye kutokana ina pesa nyingi sana iliyo weza kutolewa kama ofa”
“Kazi gani?”
“Kazi ni ya mauaji, kuna kifaranga kimoja kinatakiwa kuweza kuuwawa iwe isiwe nilazima kiuwawe”
 
“Kifaranga?”
“Ndio, siwezi kusema ni mtu kwa maana ni msichana mdogo tu makamu yangu, anamsumbua mwana mama mmoja na anahitaji msichana huyu leo hii aweze kuondolewa duniani”
Akili yangu moja kwa moja nikaipeleka hadi kwa Delfina, ila siuhitaji kumtilia mashaka kwa maana wana wekeana visasi ni wengi katika huu ulimwengu.
“Huyu msichana yupo vipi?”
Hawa akanisogezea bahasha nyeupe, nikaichukua na kuifungua kwa ndani, nikaichomoa picha iliyomo humu ndani, sikuamini macho yangu kuikuta sura ya Mariam. Nikayakaza sana macho yangu kwenye hii picha ya Mariam ambaye Vivian alisha nieleza kwamba Mariam ni mfu kwa sasa.
“Huyu binti ana mahusiano na kijana mmoja wa kitajiri hapa Somali, kijana huyo alisha andaliwa mwanamke wa kumuoa tangu kipindi alipo kuwa mdogo. Sasa huyo binti amekuja kuharibu mahusiano ya wapendanao hao wawili. Kijana haoni wala asikii kwa huyo binti. Na huyu mama aliye ileta hii picha hapa anahitaji binti huyo kuuwawa mara moja iwezekanavyo”
 
Nikajikuta nikishusha pumzi huku nikiendelea kuitazama picha ya Mariam. Hakuna kitu hata kimoja kilicho badilika katika sura ya Mariam, hapo hapa duniani binadamu ni wawili wawili, ila Mariam ninamtambua vizuri sana.
“Kwa nini mumenipa mimi hii kazi?”
Niliuliza swali la mtego ili kuweza kuyasoma mawazo ya Hawa, anafikiria kitu gani juu yangu mimi.
“Hii kazi baba ndio  aliye agiza upewe wewe, ukiifanikisha upendo wa baba juu yako utazidi kuwa karibu sana na unaweza kuwa hata mlinzi wake wa karibu”
 
“Ningeomba unipe maelezo binti huyu anapatikana wapi, ila hata kama ni kazi niweze kuifanya kuanzia muda huu”
“Nyuma ya hiyo picha kuna maelekezo ya sehemu anayo fanyia kazi kikubwa ni wewe kuhakikisha kwamba unakwenda kuifanya hii kazi, tena kwa uangalizi mkubwa sana kwa maana ninasikia kwamba huyo binti yupo vizuri kwenye maswala ya upambanaji, ndio maana watu wengi walio tumwa kumuu, waliambulia patupu”
Maneno ya Hawa yalinifanya nizidi kuamini kwamba huyu anaye mzungumzia hapa ni Mariam ninaye mfahamu mimi, kwa maana Mariam yupo vizuri sana kwenye maswala ya upambanaji.
“Basi inabidi munipatie hata siku mbili kuhakikisha kwmaba hii kazi nina ikamilisha. Kama unavyo jua, mimi sio mwenyeji wa hii nchi, na maeneo haya uliyo nieleza hapa ninatakiwa nifike kwa kutmia ramani ambayo mutanipatia”
“Usijali hilo jambo la ramani, siku za kuifanya hii kazi, basi nitahakikisha kwamba unapata kile unacho kihitaji. Kwa sasa nenda kajiandae kwa ajili ya safari, utapatiwa suti mbili, pamoja na gari moja”
 
“Pesa”
“Dola elfu tatu itakutosha kabisa kwneye hii kazi kwa maana hapa Somalia pesa yetuu haina thamani kubwa sana”
“Sawa sawa”
Nikatoka ofisini kwa Hawa na moja kwa moja nikaelea hadi chumbani kwangu. Nikaka kitandnai na kuanza kuitazama picha ya Mariam. Taratibu nijakuta nikiipeleka picha yake hadi mdomoni mwangu na kuibusu. Mwili mzima ukasisimka kwa hisia kali za mapenzi, kwa maana Mariam ni mwanamke ambaye nilimpenda mimi mwenyewe kutoka moyoni mwangu, japo mapenzi yetu yalijaa hatari za hapa na pele, bali hii ndio nafasi ya pekee mimi kwenda kuonana naye kwa mara nyingine tena.
Nikaelekea bafuni na kuoga kwa haraka, nikajiweka sawa, suti za ina mbili zikaletwa chumbani kwangu na Hawa, akanikuta nikiwa nimejifunga taulo tu kwa manaa ndio nimetoka kuoga.
“Suti hizi hapa, kitambulisho cha nchi hichi hapa. Hakuna askari atakaye kukamata na kukusumbua kuhusiana na kitambulisho”
“Asante sana”
“Funguo ya gari hii hapa, pesa nazo hizi hapa. Hakikisha hii kazi unaifanya kiufasaha. Ninakupa siku nne, nitahitaji urudi na majibu mazuri”
 
“Hakuna tatizo mkuu nitahakikisha kwamba kila jambo linakwenda vizuri kama nilivyo kusudia”
“Itakuwa ni vizuri sana. Gari ipo sehemu ya magesho, hii simu ina GPRS System itakuongoza hadi kwenye mji ambo huyu binti anapatika. Tutakuwa tunawasiliana mimi na wewe kupitia hii simu, utanipa ripoti ya chochote kitakacho endelea. Kama ni kuhitaji msaada wangu basi hakikisha unanitaarifu mapema na msaada utaupata sawa”
“Sawa mkuu”
“Vaa nguo, ninakusubiria nje”
Hawa akatoka chumbani kwangu na kurudishia mlango. Nikaichukua suti moja iliyo andaliwa na kila kitu chake kuanzia viatu, tai, shati hadi miwani. Nikavaa kila kitu sehemu inayo husika katika mwili wangu kisha nikamalizia na miwani kubwa kiasi. Nikachukau bastola yangu na kuichomeka kiunoni mwangu, nikachukua magazine nne na kuziweka kwenye mifuko ya ndani ya koti la suti. Picha ya mariamu yanyo nikaiweka kwenye koti la suti, pesa na kitambulisho changu nikaviweka mfukoni mwangu.
 
‘Muda umewadia wa kufanya kile ninacho kihitaji kukifanya’
Nilizungumza moyoni mwangu, huku nikifungua mlango wa chumba changu, nikamkuta Hawa na walinzi wake wakiwa wananisubiria. Hata hawa alivyo niona kidogo macho yake yakaonekana kuonekana kuwa na furaha kiasi japo hakuhitaji kuseme chochote kwangu. Nikaongozana naye hadi kwenye maegesho ya magari. 
 
“BMW X6 naamini itakusaidia kwenye kazi yako si ndio?”
“Ndio mkuu”
“Nikkuitakie kazi njema na mafanikio mema”
“Asante”
Gari hii nikaitazama vizuri, kwaasilimia kubwa inafanana na gari yangu ambayo nilipewa na raisi wa jamuhuri ya muunganowa Tanzania. Nikafungua mlango na kuingia.
“Hakikisha unaendesha vizuri, askari wa usalama barabarani wapo wengi sana”
“Sawa mkuu”
Nikafunga kioo cha gari na kuondoka katika eneo la maegesho ya mgari na kuelekea katika geti kuu la kutokea katika hii ngome. Nikaendelea kuendesha gari kwa umakini huku nikifwata ramani inayo onekana kwenye hii simu aliyo nipatia Hawa. Nikiwa katikati ya jangwa, ila kuna barabara ya lami iliyo nyooka vizuri nyuma, yangu nikaanza kuona gari mbili nyeusi zikija kwa mwendo wa kasi sana huku zimewasha taa. 

Wasiwasi ukanipata kidogo ila nikaendelea kuzitazama kwa umakini jinsi zinavyo zidi kuja kwa kasi, zikazidi kunikaribia, gafla gari moja ikanipita na kusimama mbele ya gari langu na kujikuta nikifunga breki za gafla gari nyingine ikasimama nyuma yangu. Wakashuka watu wawili kwenye gari la mbele wakiwa wamevalia suti nyeusi huku wakiwa na bunduki mikononi mwao. Kwa kioo cha pembeni nikatazama nyuma napo nikaona watu wengine wawili walio valia suti wakiwa wamesimama huku mikononi mwao wakiwa wameshika mitutu ya bundiki wakininyooshea mimi kwenye gari langu, jambo lililo nifanya nijiulize hawa watu wanahitaji nini kutoka kwangu.

AISIIIII……….U KILL ME 88                                                                                                 

Taratibu nikaanza kuichomoa bastola yangu sehemu nilipo iweka, ila hata kama wakianza kulete mashambulizi kwangu basi ninaweza kujilinda. Mtu mmoja kutoka mbele ya gari langu akaanza kutemeba kwa utaratibu huku bunduki yake akiwa ameninyoonyesha mimi. Alipo fika karibu na kioo cha upande wangu. Akaonekana kama kushusha pumzi nyingi na bunduki yake akaishusha chini. Akaanza kuzungumza na wezake wakionekana kulaumiana, kwa ishara wakaniomba niweze kuondoa gari langu, inavyo onekana walio kuwa wakimtafuta gari lake limefanana na mimi.
 
Nikairudisha bastola yangu sehemu nilipo ichomo na taratibu nikaanza kuondoka huku nikiwatazama kwenye kioo changu cha pembeni jinsi wanavyo geuza magari yao na kurudi walipo tokea.
Nikaendelea kufwata muelekezo wa ramani iliyopo kwenye simu yangu hadi nikafanikiwa kufika kwenye mji wa Adale ambapo ndipo ninapo elezwa kwamba ndipo anapo patikana Mariam. Huu mji umejaa Nyumba zilizo jengwa kama nyumba zinazo jengwa Iraque. Watu wengi wa hili eneo mavazi yao ni kanzu kwa wanaume na wanawake wengine wamevalia mabaibu na mitandio katika vichwa. Mji huu hauna watu wengi sana, nikatafuta moja yua hoteli ambayo ni ya kawaida, nikaegesha gari langu kwenye moja ya maegesho ya hii hoteli. Baada ya kuyasoma mazingira katika hii hoteli taratibu nikashuka kwenye gari langu huku nikiwa makini. Nikaingia kwenye mlango wa hii hoteli.
 
“Asalam Alykum”
Muhudumu wa kiume alinisalimia lugha hii ambayo ni ya kidini haswa.
“Salama, ninaimani unafahamu kiswahili?”
“Ndio ninafahamu”
“Nahotaji chumba”
“Chumba vipo unahitaji gorofani au chucha cha chini?”
“Ninahitaji gorofani, je usalama upo?”
“Upo mkuu wangu, wala usiwe na wasiwasi wowote”
“Sawa naomba, nipatie ninalipia kwa siku mbili”
Nikatoa noti ya dola hamsini na kumpatia muhudumu. Akaniomba kitambulisho changu, akaingiza jina langu kwenye computer yake, akanirudishia kitambulisho changu na kunipatia funguo ya chumba alicho nielekeza kwamba kipo gorofani. Nikapanda hadi gorofani, nikakuta kordo yenye vyumba vingi vinavyo tazamana milango. Nikaanza kutafuta namba ya chumba changu hadi sehemu kilipo, nilipo kipata nikafungua na kuingia ndani. Nikaanza kukichunguza chumba hichi  kwa umakini wa hali ya juu, kila kona kila sehemu nikaipitishia jicho, nikageuza gadi godoro. Nilipo hakikisha kuna usalama wa kutosha nikapanga kitanda changu vizuri. Nikafungua dirisha na kuanza kutazama mandhari ya nje ya huu mtaa.
 
Nikatoa simiu yangu mfukoni, nikatazama idadi ya namba zilizomo kwenye simu, nikakuta namba mbili tu, na zote zina jina la Hawa. Nikampigia na kuiweka simu yangu sikioni, simu ikaita kwa sekunde kadha kisha ikapokelewa.
“Habari mkuu?”
“Salama vipi hali  ya safari?”
“Nzuri nimefanikiwa kufika salama, na nipo kwenye moja ya hoteli. Jioni hii ndio ninahitaji kuanza hii kazi ya kumtafuta huyu msichana”
“Nashukuru kusikia hivyo hakikisha kwamba unaifanya kazi hii kwa ufasaha na umakini wa hali ya juu”
“Sawa mkuu”
“Nikutakie kazi njema na jioni njema”
“Nawe pia”
Nikakata simu, nikatoa picha ya Hawa mfukoni, nikaipiga picha kwa kutumia simu yangu kisha nikairudisha kwenye begi. Nikaka ndani ya chumba changu hadi majira ya saa moja na nusu usiku, sikuona haja ya kuvua suti hii niliyo vaa kwa maana ndio kwanza ninaianza kazi. Nikatoka katika chumba changu na kukifunga vizuri. Nikafika mapokezi na kumkuta muhudumu mwengine tofauti na muhudumu ambaye nilimkuta.
 
“Samahani kuna yule kaka aliye kuwa hapa mida ya mchana yupo wapi?”
“Ametoka shifti yake, ila bado hajaondoka hapa hotelini”
“Nitampata wapi?”
“Ngoja nimpigie”
Kijana huyu wa kisomali akanipa ushirikiano mzuri sana. Akampigia simu mwenzake huyo ambaye nina shida naye mhimu sana.
“Anakuja ninakuomba ukae kwenye vile viti”
“Shukrani kaka”
Nikaka kwenye viti vilivyopo hapa mapokezi. Haukupita muda sana kijana huyo akaja akiwa amesha badilisha mavazi yake ya kazi.
“Vipi kaka?”
Alinisalimia kwa furaha, kwa haraka haraka mtu unaweza kusema sisi ni marafiki wa kipindi kirefu sana ila ndio kwanza tumekutana leo. Ila ninavyo hisi tumetokea kuzoeana gafla sana.
“Safi ninahitaji msaada wako ndugu yangu”
 
“Msaada gani kaka?”
“Kama unavyo fahamu mimi hapa ni mgeni, ninahitaji kuzunguka zunguka kwenye huu mji”
“Hakuna tabu kaka, tena ndio nimesha toka shifti itakuwa ni vizuri sana”
“Kaka asante kwa msaada wako”
“Hakuna tabu kiongozi”
Tukatoka nje na kijana huyu moja kwa moja tukaeleka kwenye maegesho ya magari. Tukaingia kwenye gari langu.
“Kusema kweli tangu kuzaliwa kwangu, leo ndio nimepanda hili gari”
“Hahaa ni vitu vidogo mbona”
“Ahaaa kwa hapa Somalia kupanda gari kama hili ni shuhuli kubwa sana, si unajua nchi yenyewe amani  imesimamia mguu mmoja”
“Kweli, nalitambua sana hilo”
“Ila inabidi kuwa makini sana na hili gari kwa maana kuna vijana wanavijikundi kundi vyao, basi wanateka magari sana”
“Weee”
“Ohooo kweli, kazi yao wanateka magari na kwenda kuyauza kwa watu wanao yabadilisha”
 
“Sawa sawa, hapa kuna Club gani nzuri?”
“Ahaa huu mji bwana umetawaliwa sana na dini, maswala ya Club, disko disko huku, hakuna kabisa”
“Weee!!”
“Kweli kaka sikutanii, huu mji ukitaka kuuwawa siku yoyote yaani, wewe fungua baa, disko au kasino utakiona cha mtemakuni. Na hata hapa hotelini kwetu, hatulazi watu wa jinsia mbili pasipo wao kuwa na cheti cha ndoa”
“Kweli hiyo nimeipenda”
“Yaani katika miji iliyo tulia tulia huu umetulia. Ila kuna disko moja lipo nje ya huu mji, lipo jangwani, kwa maana sisi hapa tumepakana na jangwa hapo mbele tu kidogo. Ila disko hilo usalama wake ni mdogo sana”
“Tunaweza kwenda?”
“Kwenye hilo disko…..!!?”
“Ndio”
“Ahaa kaka kunipeleka huko haiwezekani kabisa, mama yangu bado ananitegemea isitoshe ni mgonjwa. Kwa hichi kidogo ninacho kipata ndio hicho hicho kinacho muuguza. Nikienda huko ninaweza kufa ikwa tabu nyingine kwa mama yangu”
 
“Kwani mama matibabu yake yanagarimu kiasi gani?”
“Haizidi hata dola mia tano, ila ishu ni kuipata hiyo pesa”
“Na kwa sasa mama yako yupo wapi?”
“Yupo nyumbani tu”
“Tunaweza kwenda kumuona?”
“Hakuna shaka”
Nikawasha gari, kijana huyu akaanza kunielekeza wapi nipite na wapi niende.
“Hivi unaitwa nani, kwa maana tume zoeana sana”
“Mimi ninaitwa Rashid, najua wewe unaitwa Dany”
“Yaa hujakosea”
“Umekuja hapa kwa kazi gani, kwa maana wengi wanoa kuja kwenye huu mji wanakuja kwa kazi maalumu”
“Unajuaje kama wanakuja kwa kazi maalumu?”
“Wenyeji wa hapa kazi yetu sisi ni kusali misikitini na kufanya kazi ndogo ndogo, nyingine kama hizo za kutunza nyumba za wageni.”
“Ahaaa”
“Simama hapo kwenye hiyo nyumba”
Rashid alinielekeza. Nikasimamisha gari langu na tukashuka, akanikaribisha ndani kwenye hii nyumba yenye mandhari ya kawaida tu. 
 
“Ngoja nimtazame mama chumbani kwake kisha nitakukaribisha uweze kumuona”
“Sawa”
Nikabaki nikiwa nimesimama kwenye kordo kwa maana hakuna chumba. Hazikupita hata dakika mbili Rashidi akatoka kasi huku akiwa anahema.
“Kaka Dany mama yangu, hali yeke ni mbaya sana”
“Ni mbaya?”
“Ndio njoo nisaidie kaka yangu tumuwahishe hospitalini”
Ikanibidi kuingia ndani ya chumba hichi, nikamkuta mama Rashid akiwa amejinyoosha kitandani huku mwili wake ukiwa umekakama. Kutokana nina nguvu kuliko Rashidi kwa haraka nikamnyanyua na kumbeba. Tukatoka nje na kumuingiza ndani ya gari. Rashida akanza kunionyesha njia za kupita hadi tukafanikiwa kufika hospitali. Menesi wakatusaidia kwa kutupatia kitanda cha wagonjwa chenye matairi. Nikamlaza vizuri katika hichi kitanda, manesi wakaanza kukisukuma kitanda hichi wakikipeleka katika chumba ambacho wataweza kutoa huduma ya kwanza kwa mgonjwa.
Rashidi hakuzungumza kitu chochote zaidi ya machozi kumwagika usoni mwake. Ikanibidi nianze kazi ya kumfariji ili ajikaze na nguvu yake aipeleke katika kumuombea mama yake.
 
“Atapona jikaze mdogo wangu”
“Asante sana kaka kwa msaada wako. Yaani Mungu ni mkubwa laiti kama ingekuwa si wewe kunichunuku mimi ninahisi sasa hivi mama yangu anguwa kwenye hali mbaya zaidi ya hii aliyo kuwa nayo”
“Usizungumze hivyo Mungu ni mwema, kila kitu kitakwenda vizuri”
Simu yangu mfukoni ikaita, nikaitoa na kukuta Hawa ananipigia.
“Ndio mkuu”
Nilizungumza kwa sauti ya chini huku nikisimama na kusogea mbali kidogo sehemua mbayo Rashidi wala mtu yoyote anaweza kunisikia.
“Kwenye hiyo hospitali  umefwata nini?”
Hapa ndipo nikagundua kwamba hii simu yangu imeunganishwa na satelaiti kila ninapo kwenda Hawa ananiniona.
“Nipo kwenye harakati za kumtafuta adui”
“Kwani umepa habari kwamba yupo hospitalini?”
“Hilo ni jibu ndio maana nikaja hapa.”
“Kuwa makini”
“Asante”
Nilijikuta nikianza kumchukia Hawa, kwa maana kwenye maisha yangu sipendi kitu kinacho itwa kufwatiliwa tena kila ninapo kwenda niwe ninaonekana. Nikaitazama hii simu nikatamani kuipasua ila ikanibidi kughairisha zoezi hili. Nikairudisha mfukoni, nikamtazama Rashidi sehemu aliyo kaa, nikamuona akiwa amekaa na kujiinamia chini. Nikaelekea sehemu ya mapokezi kwenye hii hospitali.
 
“Habari yako dada”
“Salama”
“Kuna mama tumemleta muda huu, sasa ninahitaji kulipa garama zote mimi”
“Hakuna shida kaka”
“Itagarimu kiasi gani?”
“Hadi tufahamu majibu ya daktari”
Nikatoa waleti yangu na kutoa noti sita za dola mimi mia. Nimamuwekea nesi mezani.
“Naomba risiti, endapo kutakuwa na garama nyingine zaidi basi nitahitaji munieleze”
“Sawa kaka”
Nesi akaanza kuniandikia risiti, kisha akanikabidhi. Nikatoka nje na kuelekea sehemu ya maegesho ya magari. Nikasimama kwa muda, huku nikitazama gari nyekundu aina ya benzi inayo simama pembeni yangu. Dereva wa gari hili akafungua mlamgo kidogo, na kuanguka chini, jambo lililo nifanya nibaki na mshangao, ila nilipo mchunguza kidogo, nikagundua ana jeraha la risasi kwenye kifua chake na nidamu nyingi zinazo endelea kumvuja katika jeraha lake na endepo nisipo fanya msaada wowote kwake basi anaweza kupoteza maisha mbele yangu.
                                                                            ITAENDELEA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya