Get the latest updates from us for free

mas template
Home » , » AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 83 na 84 )

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 83 na 84 )

Written By Bigie on Wednesday, April 11, 2018 | 3:06:00 PM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA-
0657072588

ILIPOISHIA   
Nikiwa katika kuwatazama tazama wanajeshi hawa wa kisomali, nikamuona kijana mmoja ambaye naye amenikazia macho. Kumbukumbu yangu ikarudi hadi siku ambayo tulikuwa Tanga na raisi, na njiani tukakutana na magari ya wasomali, na tukapambana nao na kuwaua wote. Mmoja wa vijana ambao nilipambana nao ni huyu anaye nitazama sana. Kijana huyu akasimama huku bunduki yake akiwa ameishika vizuri, akaanza kupiga hatua huku akinifwata akionekana kuwa na jazba kubwa usoni mwake. Nikatamani kufanya kitu ila uwezo sina, na kitu kingine ninaogopa sana hawa watu wakifahamu kwamba mimi nilikuwa mpelelezi nchini Tanzania na nimiongoni mwa watu nilio sababisha vifo vya ndugu zao wengi sana jambo ambalo nahisi hadi leo wameweka uhasama mkubwa na nchi ya Tanzania.
           
ENDELEA       
Cha kumshkuru Mungu hawa akawahi kumzuia kijana huyu, na wezake wawili wakakimbilia sehemu tulipo na kumkamata huku wakimpokonya bunduki yake. Hawa akaanza kuwafokea vijana hawa, walimo mkamata mwenzao kwa lugha ambayo siielewi. Wakaondoka nakijana huyu huku wakiendelea kumvuta na kumbeba juu juu.
“Samahani mwanye Dany”
“Bila samahani”
“Huyu kijana ana matatizo ya akili, kwa hiyo akiona watu wapya basi inakuwa ni shida, sana. Sasa sijui imekuwaje hadi wamemuachia akatoka nje”
 
“Ahaa kumbe”
“Yaa akili yake haipo sawa kabisa, yaani anashida sana.”
“Kwani hapo mwanzo alikuwa na hali kama hii?”
“Hapana, huyu kijana nimekuwa naye kabisa, akili zake zipo kama kawaida, ila tatizo linalojotokeza alipo okoka kufa, nchini Tanzania. Kuna kazi moja walikwenda kuifanya, basi kati ya watu wote walio kuwa wamekwenda kule yeye ndio wa pakee ambayo elinusurika kufa”
“Duuuuu”
“Yaa ndio hivyo bwana”
Hawa alizungumza huku tukiendelea kutembea taratibu akinionyesha baadhi ya maeneo katika ngome hii iliyo jekwa kwa uimara mkubwa sana. Hata ukuta wake ninaweza kuufananisha na kuta kubwa zilizo kuwepo kwenye ngome za kifalme huko nchini Italia
 
“Sasa baada ya hao wezake kuuwawa, mumeamuaje?”
“Daaa ni mpango mkubwa sana ulio andaliwa dhidi ya Tanzania, ila utaufahamu, hali yako ikiwa vizuri”
“Ahaa sawa sawa”
Nilizungumza kana kwamba sielewi kitu ambacho kinaendelea. Sikuhitaji kuuonyesha wasiwasi wangu mbele ya Hawa, kwa maana hili nalo linaweza kuwa kosa, na wala sikuhitaji kuuliza swali jengine juu ya huo mpango wao ambao wameupanga dhidi ya Tanzania. Kwa mwendo  huu wa taratibu tunao utembea tukafika sehemu ambayo kuna jishe la wasichana na wanapata mafunzo yao.
“Hili ni jeshi langu, hawa wote unao waona hapa, wapo chini ya mamlaka yangu”
Kwa haraka haraka wasichana hawa nimewahesabu idadi yao wanafika kama hamsini hivi. Mafunzo wanayo fundishwa kwenye hivi viwanja unaweza kusema kwamba si watoto wa kike kwa maana wapo kikakamavu kama wanaume. Tukaendelea kuzunguka na kuelekea maeneo mengine ya kutengenezea silaha za kivita.
“Hapa kuna wataalamu  wengi sana wa kutengeneza, bunduki, mabumo, majambia. Yaani tumejipanga kisawa sawa”
“Kweli hata mimi naona. Ila kwa nini unaniambia mimi haya yote?”
 
Nilimuuliza Hawa swali hili kwa kumtega tu, kwa maana sijaielewa maana yake ya kunieleza mimi kila kitu isitoshe hawafahamu kwamba mimi ni nani na ninamaisha gani kabla sijafika hapa.
“Ninakuonyesha haya yote kwa kuwa, hadi sasa wewe ni moja ya wanachama wa kundi la baba yangu. Na yeye ndio ameagiza mimi kukuonyesha haya yote. Naamini hadi hapo utakuwa umenielewa?”
“Yaaa”
“Naamini ukipona utajifunza haya yote ambayo wezako wanafundishwa”
“Kweli nitaweza?”
“Utaweza, wapo ambao walikuja hapa hata ngumi kurusha hawawezi, ila kwa sasa nikikuonyesha huto weza kuamini”
“Wee”
“Njoo huku”
Tukaingia kwenye moja ya ukumbi, tukakuta watu wanajifunza maswala ya kareti. Hawa akaanza kunionyesha mtu mmoja baada ya mwengine ambao kipindi wanaingia kwenye huu ukumbi walikuwa hawajiwezi kabisa katika maswala ya mapambano. Kila anaye nionyesha yupo vizuri katika kupamban.
 
“Kweli mimi ninaweza kuwa kama yule jamaa pale?”
Niliuliza huku nikimnyooshea jamaa mmoja mkono.
“Ndio, na kwa jinsi ninavyo kuona unaweza kuwa zaidi hata ya yule jamaa pale”
Siku yote hii nzima tukaimaliza katika kuzunguka katika maeneo ya hii ngome hadi tukaimaliza. Hawa akanirudisha chumbani kwangu, nikapata chakula cha ukiku na kulala. Kadri muda na siku zinavyozidi kwenda ndivyo jinsi Hawa alivyokuwa akiutumia muda wake mwingi kuwa na mimi huku akinifundisha lugha yao wanayo izungumza. Cha kumsukuru Mungu akili yangu ni mzima sana na inashika vitu kwa haraka sana. Nikaanza kuielewa luga wanayo itumia kuizungumza, ikafikia hatua na mimi nikaanza kuizungumza kwa ufasaha kiasi. Ila katika siku zangu zote ninazo kaa na hawa na kunipatia mafundisho ya luga yao sijawahi kuiona sura yake, kila siku  ni mtu wa kuificha sura yake.
“Waooo kwa sasa unaweza kuzungumza kiarbu vizuri eehee”
Hawa aliniuliza huku tukiwa tunatazama macho yetu.
“Yaaa”
Nilijibu huku nikiwa ninatabasamu pana usoni mwangu, ila kwa leo nimadhamiria kuiona sura yake. Kwa maana hadi sasa sijawahi kuiona sura yake na ni mwezi wa pili unakwenda mwezi wa tatu.
“Safi, sijawahi kuwa karibu na mtu na kumfundisha hii lugha”
“Kwa nini?”
 
“Mara nyingi huwa sipendi kuwa karibu na wanaume, ila ulivyo kuja wewe, kidogo nimejitahidi kuwa karibu na wewe”
“Unawachukia wanaume?”
“Hapana siwachukii ila sipendi tu kuwa karibu nao”
“Ninaweza kukuomba kitu kimoja?”
“Kitu gani?”
“Ni miezi sasa sijawahi kuiona sura yako, ninakuomba niweze kuiona”
Hawa akaka kimya kwa muda huku macho yake yakiwa yamebadilika na kuwa kama mtu mwenye hasira, sikulijali hilo sana kwa maana jambo lililopo moyoni mwangu tayari nimesha weza kulizungumza.
“Mtu ambaye anaiona sura yangu, ni baba yangu peke yake. Dany kwa hilo ninakuomba unisamehe”
Hata sauti ya hawa imebadilika katika kuzungumza kwake, imekuwa ya msisitizo sana, hata vicheko vyake alivyokuwa anavicheka muda mchache ulio pita vibakwisha kabisa. Hawa akasimama na kutoka chumbani kwangu. Nikabaki nikiwa na vitabu vyangu vilivyo andikwa kwa kiarabu na kutafsiriwa kwa Kiswahili.

Mguu wangu cha kumshukuru Mungu upo katika hatua za mwisho mwisho kupona. Hata jicho langu nalo lipo katika hatua za kupona kabisa kwa manaa hata bandeji ambayo ilikuwa imezunguka kichwa changu kizima, nilisha itoa wiki kadhaa nyuma. Siku iliyo fwata nikaanza kufanya mazoezi madogo madogo, hawa hata ukaribu wake na mimi ukaanza kupungua jambo  mbalo ninahisi limetokana na mimi kuhitaji kuiona sura yake. Baada ya wiki moja, mguu na jicho langu vikapona kabisa. Nikaanza mazoezi na watu ambao nao ndio wanao anza, karibia asilimi tisini na tano ya haya mazoezi tunayo yafanya ninayafahamu, ila ninajifanya mjinga nisiye jua kitu cha aina yoyote.

Mwalimu wangu wa mazozi ya kijeshi taratibu akaanza kuonyesha upendo wake kwangu, kwa jitihada ambazo ninazifanya katika kila zoezi ambalo ananipatia.
“Dany baada ya mwenzi moja mbele, ukiendelea na hii kasi yako utakuwa vizuri sana katika kupambana”
“Asante mwalimu”
 
“Huu ni mwaka wa kumi na mbili sasa ninafundisha vijana kwenye hii kambi, ila sijawahi kupata mwanafunzi asiye jua na anahitaji kujua kama wewe, kwa kweli unanipa hata moyo naamini kwamba utanifuta aibu”
“Nitakufuta aibu ya nini mwalimu?”
“Vijana wengi ambao wanatoka kwenye mikono yangu, na kwenda kufanya kazi za nje, wengi wao wanafia huko na kurudi wachache, jambo ambalo linanifedhehesha”
“Kwani tukimaliza haya mazoezi, tutapangiwa kazi?”
“Ndio nilazima mupangiwe kazi, kisha mukitoka huko ndio munakwenda kwenye hatua nyingine”
“Ahaa sawa sawa mwalimu, na kazi zenyewe zinakuwa za aina gani?”
“Inatokana na mzee atakavyo hitaji ni wapi muende kuifanya hiyo kazi. Kikubwa ni umakini tu”
“Sawa mwalimu nitahakikisha kwamba kila jambo linakwenda vizuri”
 
“Kama mutakwenda nitapendekeza wewe upewe uongozi  wa kikosi”
“Sawa mwalimu”
“Haya kapumzike ni usiku sasa”
“Asante mwalimu”
Nikaichomeka basola yangu kiunoni na taratibu nikaanza kutemebea kueleka kwenye chumba changu, bahati niliyo ipata ni kwamba nina chumba changu binafsi, ila wezangu wanalala kwenye mabweni yao kama zilivyo nyumba za bweni. Ngome imetulia na watu wanao katiza katiza ni walinzi kwa maana muda wa kulala ulisha fika. Kutokana ninajulikana kwa sasa karibia na watu wote ndani ya kambi, hakuna mlinzi ambaye alinitilia shaka. Nikafika katika mlango wa chumba changu kidogo nikaona kuna utofauti, kwani asubuhi nilivyokuwa ninatoka, kitasa nilikifunga vizuri, ila sasa hivi nimekikuta kipo wazi, inamaanisha kuna mtu aliingia na kuucha mlango wangu wazi.
   
Nikaichomoa bastola yangu kiunoni na kuishika vizuri. Kwa mwendo wa taratibu nikaanza kuusukuma mlango wangu kwa ndani, huku nikiingia kwa kunyata kabisa. Nikaingia ndani na kuwasha taa. Nikamkuta Hawa akiwa amekaa kwenye kiti ambacho siku zote huwa akakaa akiwa ananifundisha.
“Karibu”
Hawa alizungumza huku akinitazama usoni mwangu, nikaichomeka bastola yangu kiunoni na kuufunga mlango wangu kwa ndani.
“Mbona usiku wote huu?”
Hawa hakujibu kitu chochote zaidi ya kusimama. Tukaendelea kutazama kwa muda kisha mimi nikachomoa bastola yangu na kuiweka juu ya meza.
 
“Dany”
“Nakusikiliza”
“Ahaa, ahaaa”
Hawa alijing’ata na kunifanya nimtazame kwa mara nyingine tena kwa maana sikujua ni kitu gani ambacho kinamfanya ajing’ate ng’ate.
“Nakusikiliza, kwa maana nakuona siku hizi upo bize sana, ukaribu na mimi ukauvunja”
“Sio hivyo Dany, kwenye maisha yangu sijawahi kuonekana sura yangu kirahisi, na wewe ulivyo hitaji kuiona basi nilizidi kuwachukia wanaume kama swali lako ulivyo niuliza”
“Nilijua kabisa kwamba unawachukia wanaume na ndio maana sikuhitaji kuendelea kukuusumbua katika hilo, ila hapakuwa na umuhimu wa wewe kukata mawasiliano na wewe, ikiwa wewe ndio mtu uliye yaokoa maisha yangu na kunileta hapa kambini”
 
“Yes Dany hilo nalijua, nimelifikiria sana na nikaona ni ujinga, ni kwa nini niukatishe ukaribu wangu kisa sura tu”
Hawa alizungumza kwa sauti ya upole huku akinisogelea kwangu taratibu. Tukatazamana macho yetu kwa muda.
“Geuka nyuma”
“Nyuma?”
“Ndio, kama unahitaji kuiona sura yangu geuka nyuma”
Sikuwa na kipingamizi taratibu nikageuka nyuma. Nikasubiria kwa dakika moja nzima
“Geuka”
Taratibu nikageuka nyuma, macho yangu yakakutana na sura ambayo kusema kweli ni nzuri kupita maelezo, sura ya Hawa imebarikiwa vigezo vyote vya kuitwa msichana mzuri. Weupe alio nao usoni mwake, na nywele kazaa zilizo shuka usoni mwake zinazidi kumfanya kuonekana mrembo.
“Hivi ndivyo nilivyo, mimi ni mzuri sana. Uzuri huu niliuchukua kwa mama yangu, ndio maana baba yangu alinitunza kwenye maisha ya kuificha sura yangu ili nisipendwe na mwanaume wa iana yoyote na hivyo ndivyo nilivyo kua”
 
Maneno ya Hawa, yakanifanya nibaki nikiwa nimemtumbulia macho tu. Hawa taartibu akanisogelea huku akiwa ananitazama kwa macho yake yaliyo ulegevu. Sura zetu zikasogeleana kwa ukaribu sana.
“Dany sijawahi kufanya hichi ninacho kifanya kwa mwanaume wa aina yoyote, nakuomba u……..”
Hawa hakumalizia sentensi yake na taratibu akazilete lispi zake kwenye lipsi zangu, kitendo cha lipsi zetu kugusana, tukasikia king’ora cha hatari kikilia nje jambo lililo tufanye tubaki tumetazamana tusijue ni kipi tukifanye kwanza kati ya kuwahi hatari iliyopo huko nje au kupeana burudani ya uhakika kwa wakati huu.

 AISIIIII……….U KILL ME 84                                                                                                 

Hapakuwa na jinsi zaidi ya Hawa kurudi nyuma, akavaa ninja yake na kubakisa macho yake. Akazima taa kisha akatoka chumbani kwangu pasipo kuzungumza kitu chochote. Amezima taa kwa sababu haitaji kuonekana na mtu yoyote kwamba ametoka chumbani kwagu. Nikajiweka sawa na mimi kisha nikatoka huku bastola yangu ikiwa mkononi mwangu.
 
Moshi mwingi kutoka upande wa mashariki kwangu unaonekana ukipanda juu, na askari wote wanakimbilia katika hilo eneo. Na mimi nikaungana nao kwenda kujua ni kitu gani kilicho tokea kwa maana hadi sasa hivi sijasikia mlio wowote wa risasi.
‘Ohoo Yesu wangu!’   
Nilijisema kimoyo moyo pasipo kuitoa sauti yangu nje kwa maana, jengo ambalo linahifadhia chakula cha askari linateketea kwa moto mwingi sana, na kila ninaye muona hapa nje sidhani kama anaweza kuingia ndani ya jengo hilo kuokoa hata gunia moja la chakula. Kadri ya uwezo wetu tukajitahidi kuzima moto, ila uwezo wetu haukufua dafu kwani moto uliendelea kuteketea hadi majira ya saa kumi na moja alfajiri.
 
Katika kupepesa pepesa macho huku na kule, nikamuona Hawa akiwa amekaa chini, akionekana kuchoka sana kwa mawazo. Kwa hatua za taartibu nikamfwata ba kukaa pembeni yake. Ukimya ukatawala kati yetuu huku nikifikiria ni kitu gani ambacho ninaweza kumshauri kwa muda huu.
“Baba anasema nihakikishe askari wanapata chakula, na hili swala haitaji kulisikia kama limetokea ndani ya kambi yake”
Hawa alizungumza kwa sauti ya upole na iliyo jaa majonzi mengi sana.
“Hakuna akiba yoyote ya chakula?”
“Hapana, hii ndio sehemu ambayo tulikuwa tunahifadhi chakula chote, sijui hata asubuhi askari watakula chakula gani, na hata askari awe jasiri kiasi gani nilazima apate chakula kwanza ndio ujasiri wake uweze kuonekana”
“Yaaa ni kweli, na tunatakiwa kulitatua hili swala kabla haijafika saa nne asubuhi.”
“Ni nini nitafanya Dany, wakati chakula ndio hichi kimesha teketea?”
 
“Nina wazo”
“Wazo gani?”
“Nitakuonyesha”
Nikanaynyuka, kisha nikampa mkono Hawa, nikamnyanyua. Tukaongozana hadi kwenye ofisi yake iliyopo kwenye moja ya jengo kubwa ambalo ndipo anapo ishi mzee pamoja na viongozi wengine wakubwa wa hichi kikundi.
“Funga mlango”
Nilimuambia Hawa na akafanya hivyo, akasimama mbele yangu na kutoa ninja anayo vaa na kubakiwa na sura yake halisi.
“Una sura moja nzuri kwa nini tusiitumie kutafuta matani ya vyakula ambavyo vitakuwa mara mbili ya chakula kilicho teketea”
“Nitaitumia kivipi na huoni kwamba inaweza kiniletea shida kwa baba yangu?”
“Hadi hapa ulipo upo kwenye shida na baba yako. Leo majira ya saa moja kamili asubuhi kuna chakula cha wakimbizi kinasafirishwa kupelekwa kwenye moja ya Kambi yao hapa Somali”
 
“Umejuaje?”
“Ni moja ya data nilizowasikia wezangu wakizungumza mazoezini na wanavyo onekana kwamba wanafahamu ni wapi hicho chakula kinapelekwa ila kinatokea Mogadishu”
Hawa akakaa kimya huku akionekana kutafakari nilicho muambia. Akanitazama usoni mwangu kwa umakini.
“Unaweza kunitafutia hao wazungumzaji?”
“Ndio ninaweza?”
“Fanya hivyo”
Hawa akavaa ninja yake, nikatoka ofisini kwake, kwa bahati nzuri nikakutana na mmoja wa wanafunzi wezangu ambaye naye alikuwa mchangiajia mada mkubwa kwenye kuhusiana na swala la chakula cha wakimbizi.
“Yosea, mkuu anakuita”
“Mimi?”
“Ndio”
Tukaongozana na Yosea anaye onyesha kuwa na wasiwasi mkubwa, kwa maana hili swala lililo tokea hapa kambini ni kubwa na ukitegemea hadi sasa haijulikani nini chanzo au nani munzililishi. Tukaingia kwenye ofisi ya Hawa na kumkuta akiwa ameitandaza ramani kubwa ya nchi hii ya Somalia juu ya meza yake.
“Ohooo ni huyu mapepe?”
“Ndio mkuu”
 
“Ninamjua sana Yosea ni mr porojo man”
“Ila ni vyema tukamuuliza kwa ktu hichi tulicho kifikiria”
Hawa akamtazama Yosea ambaye amabarikiwa kuwa na kijimwili kidogo kidogo na ni mtu ambaye ni muongeaji sana katika hii kambi na kwa uongeaji wake wa kufurahisha watu amekuwa maarufu sana ndani yahii kambi.
“Yosea nahitaji umuelezee mkuu kuhusiana na lile swala la usafirishwaji wa chakula cha wakimbizi leo asubuhi”
“Ohoo, hilo. Mkuu swala lipo hivi, shirika la UNHCR na serikali ya Kenya wamerudisha wakimbizi wengi nchini hapa kutokana na ukimya wetu, wanaamini kwamba bado kuna amani. Chakula kingi kinanapakiwa kwenye magari leo ya shirika hilo, na kuepelekwa Afgoye. Pale kitahifadhiwa kwa ajili ya kuwagawia hawa wananchi chakula hicho. Sasa kama tunaweza basi kukipata hichi chakula hata kabla hakijafika hapo Afgoye, basi tutakuwa tumefeli na hali halisi unaiona”
Yosea alizingumza kwa msisitizo hadi Hawa akatingisha kichwa, huku sura yake akiwa ameifunika na nina amini mimi na baba yake ndio tunaifahamu sura yake. 
 
“Nimewapata hii kazi kwa haraka haraka itahitaji watu wangapi?”
“Wasio zidi kumi, mkuu. Kikubwa ni kuteka magari yake, na tunayaleta hapa na mchazo utakuwa umekwisha”
“Kuna usindikizaji wa askri?”
“Hilo ni lazima muheshimiwa, si unajua nchi yenyewe. Na wanajeshi wa UN hapo watahusika”
“Nitakwenda na nyinyi wawili pamoja na kikoasi changu, nendeni kajiandaeni”
“Sawa mkuu”
Yosea akatoka ofisini na kuniacha mimi na Hawa.
“Mbona unanishangaa, nenda kajiandae”
“Sawa mkuu”
Nikatoka ofisini huku na kueleka hadi kwenye eneo la kihifadhia silaha pamoja na mavazi ya mapambano. Nikaanza kujiandaa haraka haraka huku nikikusanya magazine za kutosha zenye silaha.
 
“Dany kuna kazi unayokwenda kuifanya?”
Mwalimu wangu aliingia pasipo mimi kumuona, sauti yake ndio imenifanya kugeuka nyuma na kumtazama.
“Ndio mwalimu. Madam amecharukwa na mimi amenijumuisha kwenye kazi”
“Ila bado hujawa fiti, japo unajitahidi kuonyesha kwamba unahitaji kufahamu zaidi mafunzo”
“Kweli mwalimu, ila kwa hali aliyokuwa nayo mkuu Hawa si rahisi kwa mimi kuweza kukataa amri yake na kama unavyo fahamu mimni nipo hapa kambini kutokana na yeye”
Mwalimu akaka kimya akionekana kuyatafakari maneno yangu.
“Munakwenda kuifanya kazi gani?”   
“Kuteka magari yanayo beba chakula cha msaada”
“Mungu wangu, hapo jeshi la umoja wa mataifa si litakuwepo?”
“Ndio mwalimu”
“No haiwezekani, utakwenda kufa bado ukiwa unahitajika kwenye hichi kikundi ngoja nikazungumze na mkuu”
“Mwalimu nakuomba usiende mkuu yupo kwenye hali mbaya”
 
“Hata yeye hapaswi kwenda kuifanya hiyo kazi, kwa maana majukumu kama hayo wanatakiwa kufanya watu wengine, hivi akipata matatizo uhahisi ni nani atamjibu baba yake. Sisi sote tulipo chini tunaweza kuuwawa”
Mwalimu baada ya kuzungumza maneno hayo akatoka kwa haraka katika sehemu hii, kutokana sijamaliza kujiandaa, sikuweza hata kumzuia. Nikajiandaa vya kutosha, risasi ambazo nimezibeba nina imani zinanitosha kabisa katika kuifanya hii kazi. Nikatoka na moja kwa moja nikaelekea ofisini. Nikaingia ndani na kumkuta mwalimu akiwa amewekewa bastola ya kichwani na Hawa huku wasichana wezake wanne wakiwa wamesimama pembeni kikakamavu kama hawaoni kinacho endelea.
 
“Sihitaji kufundishwa kwenye kazi yangu, kaa pembeni kabla sijakufumua ubongo  wako”
Maneno ya hawa yanaashiria kabisa amekasirika. Taratibu mwalimu akajisogeza pembeni. Hawa akairudisha bastola yake kiunoni na kutoka nje, sisi sote tukamfwata nyuma na kumuacha mwalimu ndani ya hiyo ofisi.
Tukafika nje na kukuta gari mbili ambazo dereva wake ni wasichana zimesha washwa tayari kwa kuondoka eneo la hii ngome. Gari hizi aina ya PICUP, nyuma zina bunduki kubwa ambayo imetengenezewa vyuma maalumu vya kuzuia risasi kwa mpigaji pale anapo itumia. Tukapakia nyuma, huku Hawa na baadhi ya wasichana wakipanda mbele.

Kama kawaida yetu, ni lazima nyuso zetu zifunikwe na vitambaa maalumu, ili kuficha sura zetu na ndivyo tulivyo fanya. Yosea yupo kwenye gari jengine na mimi huku nyuma nimepanda na msichana mmoja wa kikosi cha Hawa. Geti kubwa la hii ngome likafunguliwa na safari ya kuelekea nje ikaendelea. Kwa mara ya kwanza leo ndio ninatoka nje, na sehemu ambayo ngome yetu ipo ni katikati ya jangwa, hakuna mti wala nyumba na sehemu kubwa imetawaliwa na vilima vilima vya mchanga. Hapa ndipo nikagundua hata kazi nyengine ya hivi vitambaa ambavyo tumejifunga kwenye nyuso zetu, kumbe vina zuia mchanga kuingia machoni.

Madereva wanao endesha hizi gari ninaweza kusema kwamba ni wenda wazimu, kwa maana gari wanaziendesha kwa kasi kubwa sana, kinacho saidia ni kwamba eneo zima halina barabara zaidi ya machanga ndio maana madereva wanafanya hivi. Binti niliye kaa naye yupo kimya muda wote, akiitazama tazama bunduki yake, nikatamani kumsemesha ila nikaona hapa nisilete unoko nikiwa kwenye kazi mambo yanaweza kunibadilikia na kuwa mabaya bure jambo ambalo sihitaji kulioa kwa muda huu. 
 
Gafla gari zikasimama kwenye moja ya kilima cha mchanga. Hawa na wasichana wawili wakashuka. Kwa kutumia darubini zao, wakaangalia eneo la mbali sana ambalo si rahisi kwa macho ya kawaida kuweza kuona. Sikujua wameona kitu gani, walicho kifanya ni kurudi kwenye magari na safari ikaendelea.
Hatukwenda umbali mkubwa gari zikapunguza mwendo na kusimama kabisa. Watu wote tukashuka kwenye magari. Hawa akachukua darubini yake na kutazama tazama, kisha kwa ishara ya mkono akaniita mimi na kunikabidhi darubini yake. Nikaiweka machoni mwake, kwa mbali nikaona magari makubwa aina ya Scania, sita na yenye matela yakiwa yameongozana na yanakwenda kwa mwendo wa kawaida katika hili jangwa, huku mbele kukiwa na gari mbili za jeshi na nyuma ya magari hayo kukiwa na gari nyingine za wanajeshi wa umoja wa mataifa UN.
 
“Ni wakati wa kufanya ambushi sawa”
“Ndio mkuu”
“Rudini kwenye magari, kazi inaanza. Wanne gari moja na watatu gari nyingine”
Kauli ya Hawa ikatufanya tugawanyike kwa bahati nzuri mimi nikapanda naye gari moja ambapo tupo watatu, dereva yeye na mimi ambaye nipo nyuma ya bodi nikiwa nimeshika bunduki hii kubwa iliyopo kwenye gari. Yosea na wasichana wengine wamepanda gari jengine. 

 Kila gari likapita upande wake, sisi tukaeleka mbele ambapo tunakwenda kuuzuia huu msafara, huku gari jengine likielekea nyuma kuufunga msafara. Kwa mara nyingi nilisha wahi kuona filamu za kimarekani wakiwa na wasomalia na tabu zote wanazo pata waigizaji wa kimarekani kwenye hizo filamu zao, na hichi tunacho kwenda kukifanya ninaona kama nipo kwenye filamu ila nipo kwenye uhalisia wenyewe. Hatukuchukua muda, gari letu likawa limesha fika kwenye barabara ya mbele, umbali kidogo kutoka ulipo msafara. 

Hapakuwa na swala la kusubiria amri au kusubiri wafike karibu. Hapo hapo tukaanza kushambulia gari za wanajeshi wa umoja wa mataifa. Gari zote zikasimamishwa na wanajeshi wakajitahidi kupambana nasi ila hakuna kitu kibaya kwenye maisha ya ulinzi kama kuwahiwa na hichi ndio kitu ambacho kinatusaidia. Tulipo  hakikisha wanajeshi tumewadhibiti na kuwaua wote nata maderava wa magari haya tukaalisogelea gari moja na kulifungua kwenye moja ya kontena. Tukakuta shehena kubwa ya chakula ikiwa impengwa vizuri kwa mfumo wa vigunia. 

 Tukiwa katika kutazama chakula kilichopo kwenye makontena haya, kwa mbali tukasikia milio ya helicopter za jeshi.  Haikupita hata dakika mbili, helicopter mbili zikawa zimefika aneo la tukio na tukaanza kushambuliwa kutokea juu, jambo ambalo likaanza kutupa wakati mguu sana na kumchanganya kila mmoja aliyopo katika hili eneo hususani Hawa ambaye alisha anza kusherekea ushindi wa chakula hichi kingi kupita hata kilicho teketea kwenye ghala la chakula.
                                                                            ITAENDELEA   

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts