AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
Niliwauliza baada ya kuona mshangao wao unazidi, kidole kimoja cha nesi mmoja kikaniashiria nigeuke nyuma yangu kuangalia kitu kinacho toka kwenye droo nililo lifungua.Nikageuka kwa haraka, sikuamini macho yangu, hii ni baada ya kukutana na mtu niliye fanana naye kuanzia juu hadi chini, isitoshe nguo zake na zangu zimefanana sana, jambo lililo nistua kupita maelezo.Akaanza kupiga chafya nyingi, nikastukia kishindo nyuma yangu, nikageuka na kumkuta nesi mmoja akiwa ameanguka na kupoteza fahamu huku mlinzi naye akifwatiakuanguka na kukaa kimya
“Mambo Eddy”
Jamaa alinisalimia, na sauti yangu inafanana sana na sauti yangu, nikabaki mdomo wazi nisijue nini nimjibu
ENDELEA
Jamaa akatoka kwenye droo ya kuhifadhia maiti na kusimama karibu yangu, mwili mzimwa ukaanza kunitetemeka kwa maana katika maisha yangu sijawahi kukutana na vihoja kama hivi japo kuna matukio mengi ya kutisha yalisha wahi kupita kipindi cha nyuma ila la mtu anaye fanana na mimi kwangu limekuwa ni laajabu sana
“Usishangae sana”
Alizungumza huku akielekea walipo simama dokakta na nesi, akawatazama mlinzi na nesi ambao wamepoteza fahamu kisha akaachia tabasamu pana kidogo
“Hawa nao kilicho waangusha ni nini?”
Swali lake hapakuwa na mtu aliye lijibu zaidi ya sisi sote kubaki kimya tukimtazama, akachuchumaa na kumshika mlizi kichwani, gafla mlinzi akaanza kutoa chafya zilizo pelekea akazinduka na kukaa kitako na macho ya mlinzi yakabaki kuwa na mshanga kati yangu na Eddy mwenzangu.Macho yangu yakatua kwenye suruali ya dokta na kukuta ikiwa imelowa maeneo ya mbele, ikiashiria ameshindwa kuibana haja yake ndogo kutokana na woga wa kukutanan na jamaa.Akamshika nesi kama alivyo fanya kwa mlinzi na neshi fahamu zikamrejea na kuzinduka.
“Ninaamini nyinyi nyote mutakuwa munashangaa kwa nini mimi nipo hivi, jina langu ninaitwa Eddy ni pacha wa Eddy yule pale”
Eddy alizungumza huku akiwatazama manesi, akangeukia kisha akamshika bega dokata ambaye hadi sasa hivi mwili wake wote namtetemeka mithili ya mtu aliye pigwa shoti
“Mzee usiogope sana, mimi sio mtu mbaya, ila kazi yangu ni moja tu.Nimekuja kumsaidia Eddy katika swala zima la kumrudisha mke wake ambaye hajafa kama munafyo fikiria nyinyi, ndio maana kwenye droo muliyo muweka hamjamkuta”
“Amekwenda wapi?”
Nilimuuliza kwa kujiamini
“Eddy hilo swali nitakujibu baadaye na si mbele ya hawa watu”
“Jamani enendeni kwa amani ya bwana, ila hakikisheni hamuitoi siri hii ya kwamba kuna Eddy wawili.Yoyote atakaye toa siri hii basi atadili na mimi na sio Eddy yule sawa”
Jamaa alizungumza kwa sauti ya ukali kidogo, na kuwafanya dokta na watu wake kutingisha vichwa kwamba wameelewa, akawaruhusu watoke ndani ya jengo la kuhifadhia maiti, wote wakatoka wakiwa wanakimbia kila mmoja akijaribu kuwahi kufika mlangoni na asiwe wa mwisho.Baada ya dokata na watu wake kutoka, Eddy akanifwata sehemu nilipo simama na kunishika bega
“Niambie ndugu yangu”
“Safi” nilijibu hiyo basi ila kwa mbali woga umenitawala
“Pole sana na matatizo”
“Nimeshapowa ndugu yangu”
Tulizungumza huku tukielekea nje, tayari kulisha anza kupambazuka, tukaanza safari ya kuelekea kwangu huku tukitembea kwa miguu cha ajabu njiani watu hawatushangai na mara nyingine baadhi ya watu walinisalimia mimi mwenyewe
“Mbona wewe hawakusalimii?”
“Mimi hawanioni, wakiniona watajikojolea kama yule dokta”
“Umefanya fanyaje hadi hawakuoni?”
“Ni mimi mwenye ndio najua jinsi nilivyo fanya, ila usiwe na shaka utajua tu”
Kwa njia za mkato, tukafika kwangu na moja kwa moja tukaingia ndani, tukakuta baadhi ya watu walio hudhuria kwenye sherehe wakiwa wamejilaza sebleni, wakisubiria kupambazuke waende makwao, wengine wakiwa na shahuku ya kutaka kujua hali ya mke wangu inaendeleeja
“Kaka Eddy shem anaendeleaje?” Jamaa mmoja aliniuliza baada tu ya kukaa kwenye sofa
“Muambie anaendelea vizuri”
“Anaendelea vizuri”
“Pole sana kaka”
“Asante”
Baadhi ya watu wakaanza kunihoji hiji maswali kadha na kila aliye niuliza swali, alijibiwa na Eddy mwenzangu huku wote wakiamini kwamba mimi ndio ninao wajibu maswali yao.Waalikwa wote wakondoka mida ya saa nne asubuhi na tukabaki mimi na Eddy
“Ngoja nifanye usafi wa nyumba”
Eddy alizungumza na kuanza kufanya usafi wa nyumba nzima, kitu kingine kilicho niacha hoi ni jinsi kasi aliyo itumia kuisafisha nyumba yangu, hapo ndipo nikaamini kwamba jamaa sio mtu wa kawaida
“Unashangaa nini?”
“Nashangaa jinsi ulivyo safisha jumba lote hili ndani ya muda mchache!!”
“Usishangae sana”
“Wewe ni nani haswa kwa maana sijakuelewa hadi sasa hivi japo unafanana na mimi?”
Eddy akaanza kucheka kicheko kikali kilicho anza kuyaumiza masikio yangu, alipo gundua ananiumiza masiko yangu akajifumba mdomo na kuandelea kucheka ndani kwa ndani
“Mimi ni Eddy, ila nimetoka sayari nyingine na sio duniani”
“Sayari gani?”
“Marsi, hii ni sayari ambayo inasadikika kwamba watu wanaweza kushi si ndivyo?”
“Sina uhakika”
“Una uhakika gani, wewe si ulikuwa mwalimu wa Sayansi au umesha jisahau?”
“Yaa nilikuwa ni mwalimu ila sio kama nilikuwa ninafwatilia maswala hayo”
“Basi ukweli ni kwamba sayari ya Marsi watu wanaweza kuishi, ila si watu kama nyinyi”
Eddy alizungumza huku akijirusha kwenye sofa na kupandisha miguu yake yenye viatu juu ya meza ya kioo
“Watu wote wanao ishi kule wanauwezo wa ziada, na kama maishani mwako ulishawahi kusikia viumbe vyenye uwezo mkubwa wa akili kupita binadamu wanaitwaje?”
“Ellians”
“Ndio, mimi ni miongoni mwao.Kipindi nipo kwenye matembezi yangu ya kuizunguka dunia kwa bahati nzuri nikakuona wewe, ukiwa unafanana na mimi, isitoshe hadi jina tukawa tunaonana.Usiku nilikuona jinsi unavyo muhangaikia mke wako, ulivyo pambana na wale mabinti ila wale ndio walio muiba mke wako kipenzi”
“Tutampata vipi mke wangu?”
“Mke wako yupo mbali sana na hapa, hayupo chini wala hayupo juu”
“Sijuakuelewa vizuri, hayupo chini wala juu kivipi?”
“Kwa sasa huwezi kunielewa, ila kikubwa ambacho ninataka kukifanya kwako ni kuitoa hiyo pumzi uliyo pandikizwa”
“Ukiitoa si nitakufa?”
“Ndio utakufa, kwani unaogopa kufa”
Sikumuelewa Eddy ana maana gani na kila nilivyo mtazama mwenzangu hakuwa na wasiwasi hata kidogo, gafla akasimama na kuanza kunifwata katika sehemu ambayo nimesimama, nikajaribu kurudi nyuma ila akaniwahi kuukamata mkono wangu, gafla nikastukia nikirushushwa na kujibamiza kwenye ngazi na giza kubwa likatawala kwenye macho yangu, na kukaa kimya
***
Mwanga mkali ukaanz akupiga kwenye macho yangu, nikayafumbua macho yangu na kukutaa na sura ya Eddy akinitazama
“Karibu tena kwenye uhai, Eddy”
Nikajaribu kuinuka ila nikashindwa, nikajitazama pembeni na kukuta nikiwa nimefungwa kwenye kitanda, na mikanda migumu sana ambayo sio rahisi kwangu kunyanyuka, akaisogeza taa ambayo inanimulika usoni
“Unajisikiaje?”
“Vizuri”
Nikatizma pembeni na kukuta watu sita wali valia mavazi meupe wakiwa wamesimama, sura zao tofauti kidogo na binadamu wa kawaida kwani vichwa vyao ni vikubwa kiasi na wanamacho makubwa, ila pia zao ni zakawaida na hata midomo yao ni yakawaida
“Eddy hao ni kina nani?”
“Hao ni madaktari ambao wamekufanyia, huduma ya kukutoa pumzi ya kinyoka na kukuwekea pumzi ya binadamu wa kawaida”
Madaktari hao wakatabasamu, na mimi nikaonyesha tabasamu, Eddy akazungumza nao kwa lugha ambayo sijawahi kuisikia hata siku moja kwenye maisha yangu.Wakanisogelea na kuifungua mikanda walio nifunga, Eddy akanipa mkono na kunyanyuka na kukaa kitako kitandani
“Pole Eddy”
“Asante”
Nilimjibu kwa sauti iliyo jaa furaha kwani, hali ninayo jihisi ni tofauti na pale nilivyo kuwa awali, macho yangu yakazunguka kwenye chumba kizima, ambacho kimejaa mitambo ya ajabu ajabu nisiyo wahi kuiona
“Eddy usishanga sana, hapa upo kwenye jengo la hospitali yetu sisi”
“Ni duniani kweli huku?”
“Hapana ila nitakurudisha duniani, huku ndipo ulipo mji wetu sisi ma elians”
Eddy akaanza kunitembeza kwenye maeneo ya jengo hili la hospitali lililo jengwa kwa vyuma vitupu, watu wake ni waajabu sana, kiasi kwamba muda mwengine nilijikuta nikiogopa
“Eddyunatambua kwamba imetuchukua muda wa mwaka mzima hadi wewe kurudi katika hali ya kibinadamu”
“Weee!!”
“Ndio, na haikuwa kazi ndogo kuifanya”
“Eddy asante sana”
“Usijali, ila kuna watu wezangu unatakiwa kwenda kuwapa shukrani”
“Kina nani hao”
“Utawaona”
Tukaingia kwenye moja ya jengo lenye mnara mrefu, tukaingia kwenye moja ya chumba na kukuta suti nyingi nzuri, Eddy akaniomba nichague suti nitakayo ipenda, nikachagua suti nzuri nyeusi, iliyo nipendeza sana.Tukatoka kwenye chumba na kuelekea kwenye majo ya lango kubwa lililopo humu ndani ya hili jengo na kuingia ndani nikashangaa kukutana majitu makubwa yenye misuli iliyo kaza vizuri, japo sura zao ni zakutisha ila inanibidi kuwazoea tuu, tukapita katikati yao na kwenda kusimama mbele ya mtu mmoja aliye kaa kwenye kiti kikubwa cha dhahabu tupu
“Huyu ni mkuu wa jeshi la Ellians wote ulimwenguni na nibaba yangu mzazi”
Eddy alizungumza huku akiinama kwa kusujudia, ikanibidi na mimi kufanya hivyo, mkuu huyo akasimama na kutuamuru sisi kusimama.Akatusogelea na kunipa mkono mimi huku akitabasamu, nikampa mkono wangu na akaanza kuutingisha huku akitabasamu
“Karibu sana bwana Eddy”
“Asante”
“Kuna zawadi yako tumepanga kukupatia”
“Zawadi?”
“Ndio”
Akaniachia mkono wangu, akapiga kofi moja na watu wate wakapiga goti moja na kusujudia, tukabaki tukiwa tumesimama sisi watatu, mlango mmoja mkubwa ulio tengenezwa kwa dhahabu ukafunguliwa, kundi kubwa la wasichana walio valia mavazi meupe wakatoka, na kuanza kutembea mwendo wa taratibu.Wakasimama mbele yangu na wote wakaipiga goti moja chini na akabaki mmoja wao akiwa amesimama na amevalia shele kubwa huku sura yake ikiwa imefunikwa
“Nenda kamfunue”
Eddy alizungumza, nikamtazam Eddy usoni, akaachia tabasamu pana.Nikapita katikati ya wasichana walio inama chini.Nikasimama mbele ya msichana, taratibu nikamfunua kitambaa kilicho ziba sura yake, sikuamini macho yangu baada ya kukuta ni Rahma akiwa amepabwa vizuri sara yake
“Rahma!!”
“Eddy!!”
Tukakumbatiana kwa furaha huku machozi ya furaha yakianza kutumwagika kwenye sura zetu, hatukuona aibu yoyote taratibu tukaanza kunyonyana midomo yetu,
“Mmmm”
Mguno wa baba yake Eddy ukatufanya tuachiane huku sote tukiwa na furaha sana.
“Eddy mke wako tulimuokoa kutoka mikononi mwa mabinti walio kuwa wamemteka, na tulifanikiwa kuwaangamiza mabinti wote na kwasasa mutaishi kwa amani na furaha kwenye maisha yenu”
“Asante sana baba”
Nilizungumza huku machozi ya furaha yakinimwagika usoni mwangu.Akatuomba tumsogelee sehemu alipo simama, akaishika mkino yetu kwa pamoja kisha akamnyooshea Eddy mkono, Eddy akatoa visanduku viwili vidogo mfukoni mwake na kumkabithi baba yake, akatupa kila mmoja kisanduku chake na kutuomba tuvifungue.Macho yetu yakakutana na pete za dhahabu ambazo zinag’aa sana
“Munaweza kuvishana pete hizo”
Alizungumza, nikachukua pete iliyopo kwenye kisanduku changu na kumvisha Rahma, kisha Rahma naye akanivisha pete, shangwe na kelele za watu waliopo kwenye ukumbi huu zikatustua sote mimi na Rahma, maua mengi kutoka juu ya dari la jengo hili yakaanza kumwagika katika eneo zima la ukumbi.Machozi ya furaha yakaendelea kumwagika katika nyuso zetu zilizo jaa furaha.
“Nawatangaza rasmi kwamba mumekuwa mke na mume”
Baba Eddy alizungumza na shangwe zikaendelea.Eddy akatuchukua hadi kwenye moja ya kifaa cha kushangaza na kutomba tuingine sote wawili
“Jamani, ninawarudisha duniani”
Eddy alizungumza huku akikiwasha kifaa hicho, safari ya kwenda duniani haikuchukua muda sana kutokanana kifaa tulicho kipanda kwenda kwa mwendo mkali sana.Akatufikisha hadi kwenye eneo la jumba letu, tukashuka sote watatu na kukuta nyumba za taa zikiwa zimewashwa kutokana ni usiku
“Karibuni ndani”
Eddy alitukaribisha ndani, tukaingia hatukuamini kukuta nyumba yetu ikiwa imepabwa vizuri na kuwekwa vitu ambavyo kusema ukweli vimezidi kuipendezesha nyumba yetu
“Eddy na Rahma nninawatakia maisha mema”
Eddy alizungumza huku akiwa ametushika mikono yetu
“Muishi kwa amani na upendo, na watoto mutakao wapata siku moja moja nitakuwa ninakuja kuwatembelea”
“Hata wewe ninashukuru kwa msaada wako wote ulio tupatia”
Eddy akatukumbatia, akatuachia na kutoka nje, akaingia kwenye kifaa chake ambacho si kikubwa sana, na hakina mlio, akatupungia mkono wa kutuaga na kuondoka zake, nikambebe Rahma hadi gorofani kwenye chumba chetu, sote tukabaki tukishangaa baada ya kukuta chumba kikiwa na kitanda kikubwa kilicho tengenezwa kwa madini ya dhahabu huku kwenye ukuta kukiwa na picha yetu kubwa iliyokuwa ikituonyesha jinsi tulivyokuwa tunavishana pete, sakau nzima imejaa noti nyingi za dola mimi za kimarekani
“Eddy hii picha imefikaje hapa?”
“Hata mimi sijui”
“Na hizi el..”
Sikumpa ruhusa Rahma kuzungumza chohota, nikawahi kuinyonya midomo yake na sote tukaangukia kitandani na kuanza kuchojoana nguo moja baada ya nyingine, kama kawaida yetu tukaanza kupeana ile kitu roho inapenda huku kila mmoja akiwa na furaha ya utamu wa mwenzake
“Eddy”
“Mmmmm”
“Unajua kuwa mimi ndio nimekufundisha mambo haya”
“Nenda zako huko”
“Kweli”
Rahma alizungumza kwa utani huku akinikalia kiunoni mwangu na kuendelea na kupeana raha zetu.
Bada ya mwezi mmoja Rahma akaanza kuona dalili za ujauzito jambo liliozidi kujenga furaha ya upendo kati yetu, kazi yangu kubwa ikawa ni kumpeleka mke wangu cliniki kila kipindi cha yeye kwenda cliniki kilipo fika.Kipindi cha miezi ya Rahma kujifungua nikawadia, nikamkimbiza hospitalini kujifungua.Madaktari wakaniomba nisubiri nje ya chumba cha kujifungulia baada ya muda mlango ukafunguliwa
“Bwana Eddy, hongera sana”
Dokta zalizungumza huku akivua gloves zake mikononi na kujikuta nikiwa ninashauiku ya kutaka kujua ni nini dokta anataka kuzungumza
“Mke wako amejifungua salama, na amejifungua watoto mapacha wa kike, wanaafya nzuri na kilo za kutosha tu”
“Kweli dokta”
“Ndio, na mke wako amevunja rekodi ya hospiali yetu kwani haijawahi kutokea mwanake kuzaa watoto mapacha wenye kilo zaidi ya nne”
“Weeee!!! Naweza kumuona mke wangu na wanangu?”
“Ndio unaweza”
Dokta akaniruhusu kuingia ndani ya chumba ambapo nikamkuta Rahma akiwa amewabeba watoto wetu, Rahma alipo niona akaachia tabasamu pana huku akitabasamu, akanikabidhi watoto niwabebe, watoto watu wamechukua kila kitu kwetu, nywele zipo kama za mama yao ambaye ni muarabu, huku nyusi na macho yao yakiwa kama yangu.Mke wangu akakaa hospitali kwa kipindi cha wiki mbili tukaruhusiwa kurudi nyumbani, ambapo Rahma akwasiliana na wazazi wake wakaja kutoka Dubai, kila mmoja akafurahia kuona watoto watu ambao kadri siku zilivyo zidi kwenda ndivyo jinsi walivyo zidi kuwa wazuri na afya nzuri
“Eddy unapendekeza waitwe majina gani?”
Rahma aliniuliza siku kadhaa kabla ya kwenda kuwabatiza
“Kurwa aitwe Xaviela na doto aitwe Xaviena”
“Sawa mume wangu”
Siku ya kuwabatiza watoto wetu ikawadia, sikuamini kuona watu wengi wakiwemo waandishi wa habari wakijumuika nani katika sherehe ya kuwabatiza watoto watu ambao kila mtu, anahamu ya kuwaona wengine wakitamani hata kuwashika jambo lililozidi kuifanya familia yangu kuwa maarufu katika jiji zima la Tanga na Tanzania kwa ujumla
“Mume wangu kweli TANGA RAHA”
Rahma alizungumza huku akiwa amembeba Xaviena
“Kwa nini?’
“Tazama watu walivyo kusanyika kwa kutuunga mkono sisi”
“Yaa wanupendo na sisi na watoto wetu”
Nilizungumza kwa furaha huku nikimrusha rusha Xaviela ambaye muda wote anatabasamua usoni mwake
“Nakupenda sana baba Xavina”
“Hata mimi pia ninakupenda sana mama Xaviela”
Nikampiga busu la mdomoni mke wangu kama ishara ya upendo kati yetu, jambo lilio fanya watu wengi kupiga makofi huku wakishangilia kwa furaha.
MWISHO
Post your Comment