Get the latest updates from us for free

mas template
Home » , » TANGA RAHA- Sehemu ya Arobaini na Tisa ( 49 )

TANGA RAHA- Sehemu ya Arobaini na Tisa ( 49 )

Written By Bigie on Friday, April 6, 2018 | 4:54:00 PM

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA

Regina alizungumza huku akilisogelea friji moja na kulivuta nje, na kwakusaidiana na wezake, wakautoa mwili ambao hadi wanauweka chini nikabaki nikiwa ninashangaa kwani ni mwili wangu wote.
“Huyu ni wewe,  halisi baada ya kufa wakakuleta huku ila wamejisahau na kujua wewe upo hai”
Regina alizungumza huku akiugeuza mwili wangu, ambao hauna nguo hata moja, nikaliona jeraha la kisiki kilichokuwa kimenichoma mgongoni, kipindi mkia wa joka kubwa ulivyokuwa limenipiga na kunirusha juu na kukiangukia kisiki hicho
“Jile mwenyewe, sasa au unataka tukuwekee rost kama la wengine ulio wala?”

ENDELEA
Nikashusha pumzi nyingi huku nikimtazama, Regina na wezake anao fanana nao.
“Moja, mbili, ta…..”
“Ngoja kwanza Regina”
“Ehee unsemaje?”
“Ninakuomba umsaidie mke wangu, hapa nilipo sijielewi kabisa, tafadhali ninakuomba ndugu yangu”
Regina wote watatu wakaanza kucheka kwa dharau huku wakianza kunizunguka kwa kasi sehemu ambayo nimechuchumaa na mwili wangu, ninaoa ambiwa niule.Wakasimama gafla huku macho yao na sura zao zikianza kubadilika, macho yao yamejaa miale ya moto iliyo ambatana na machozi ya damu, huku sura zao zikianza kusinyaa na kuwa nyeusi tii kama mkaa.
 
“KULAAAA”
Regina mmoja alizungumza na kunifanya niitazame maiti ya mwili wangu, nikajikuta nikisimama kiujasiri huku nikiwatazama Regina wote watatu, nikamtazama aliye shika kichupa chenye dawa, wakendelea kunitazama kisha nikachuchumaa chuni, na kuishika miguu ya maiti yangu, nikaibana vizuri kwa viganja vyangu, kwa kutumia nguvu zangu zote nikainyanyua haraka na kuizungusha, ikawapiga kwenye miguu yao na wote wakaanguka chini, aliye shika kichupa chenye dawa akakiangushia karibu yangu.

Nikajirusha kwa haraka na kukiokota kichupa, na kuanza kukimbia kuelekea nje, kabla sijafika mlangoni nikastukia kumuona Regina mmoja akiwa amesimama mbele yangu.Huku sura yake ikiwa imekasirika sana, akajaribu kunirukia ila nikamkwepa na kunipa nafasi ya kutoka nikiwa ninakimbia kuelekea kwenye jingo alipo mke wangu Rahma.

Hata mimi mwenyewe nikaanza kujishangaa kwa maana mwendo wangu wa kukimbia upo kasi sana, kuwazidi wao, nikafika kwenye mlango wa kuingilia kwenye jengo alipo ingizwa Rahma, Regina na wezake wakasimama na kuninyooshea kidole, huku mmoja akinifanyia ishara ya kunichinja kichwa change.Nikatoa kitambaa mfukoni mwangu na kujifuta damu zilizopo mdomoni mwangu
 
Nikaanza kupiga hatua za haraka kwenda kilipo chumba, kitendo cha kujitokeza kwenye kona nikamkuta dada mmoja ambaye tulifika naye hapa hospitalini kipindi tunamleta Rahma, nikamkuta akiwa amekaaa chini huku analia kwa nguvu, huku baadhi ya rafiki zangu wakiwa, wanajifuta machozi kwa vitambaa vyao.Wasiwasi mwingi ukaanza kunijaa moyoni mwangu, nikaanza kupiga hatua za haraka, na kujikuta zikichanganya na kuzaa mwendo wa kukimbia hadi nikafika kwenye mlamgo wa chumba alichopo Rahma, sikumuuliza mtu zaidi ya kushika kitasa, nikafungua mlango na kukuta chumba kikiwa hakina mtu hata mmoja, mapigo ya moyo yakazidi kwenda mbio, nikatoka nje huku machozi yakianza kunilenga lenga
“Y..uuu..po wapi mke wangu?”
Niliuliza kwa kigugumizi kikubwa, na kuwafanya rafiki zangu, kuzidi kulia, hakuna ambaye aliweza kunijibu kitu cha aina yoyote.
 
“YUPO WAPI MKE WANGU”
Nilizungumza kwa sauti kubwa iliyo changanyikana na hasira kali sana, huku nikimshika rafiki yangu mmoja na kukandamiza ukutani
“Ame…”
Jamaa alichindwa kuimalizia sentesi yake, na kujikuta akimwagikwa na machozi mfululizo, moyo wa uchungu ulio ambatana na machozi yenye hasira ndani yake, vikautawala mwili wangu.Nikaanza kupiga hataua za kuelekea ilipo ofisi ya dakteri aliye niita mara ya kwanza, kabla sijafika ofisini mwake, nikawaona manesi wa ne wakisukuma kitanda kimoja, ambacho juu yake amelala mtu aliye funikwa kwa shuka la kijani, kuanzia miguuni hadi kichwani mwake.Nikahairisha safari, na kuanza kukimbilia kwenda walipo manesi.Mmoja wao akaniwahi kunizuia nisikifikie kitanda, ila nikamsukuma na akaangukia pembeni na kuwafanya wezake kubaki wakiwa hawana la kufanya
 
Nikalishika shuka na kulifunua na kukuta maiti ya bibi mmoja mzee akiwa tayari amesha fariki dunia, nikabaki nikiwa ninashangaa sana.
“Kwani kaka vipi?”
Nesi mmoja aliniuliza
“Mke wangu yupo wapi?”
“Mke wako, anaitwa nani?”
“Anaitwa mke wangu”
Hata jina la Rahma nililisahau kichwani mwangu kwa jinsi nilivyo changanyikiwa, nikaachana na manesi na kuendelea na safari yangu kwenye ofisi ya madaktari, nikazidi kutembea kwa haraka hadi ninafika nje ya ofisi nikakutana na daktari akitoka huku akiwa amechoka
 
“Doktar mke wangu yupo wapi?”
“Tulia kwanza bwana Eddy”
“Doktar hivi unielewi nimekuambia mke wangu yupo wapi, kama amefariki ninaomba munionyeshe maiti yake”
“Bwana Eddy tafadhali ninakuomba utilize jazba kwanz…”
Sikumruhusu daktari kuimalizia sentesi yake, nikalishika koti lake sehemu ya kifua na kumgandamiza ukutani
“Mke wangu yupo wapi?”
Nilizungumza kwa sauti nzito na kumfanya daktari kuanza kutetemeka, mwili mzima, hata miwani aliyo ivaa ikaanguka chini.
“Tumeshiindwa kuuuu…okoa maisha ya mke hadi ametutoka duniani”
Taarifa ya daktari ikanistua sana na kujikuta nikumuachia, mwili mzima ukahisi umepatwa na mstuko kama nilio upata siku ya kifo cha wazazi wangu walipo kufa shambani, machozi yakazidi kunitiririka mfululizo na kujikuta nikiwa nimekaa kwenye benchi lililopo pembeni ya mlango wa kuingilia kwenye ofisi ya daktari.
 
“Eddy tulijitahidi kadri ya uwezo wetu kuyaokoa maisha ya mke wako ila tukashindwa”
“Pia mke wako alituomba sana tukutafute, azungumze maneno ya mwisho na wewe ila hatukuona, na hatukujua ni wapi alipo”
Maneno ya daktari wala sikuyatilia msisitizo zaidi ya kuyatazama machozi yangu yanayo mwagika chini, kwenye sakafu.
“Mwili wake upo wapi?”
“Tuliupeleka mochwari”
“Twende ukanionyeshe”
“Labda asubuhi, kwa sasa ni ngumu kwenda mochari”
“Twende ukanionyeshe sawa”
Nilizungumza kwa msisitizo, hadi daktari akanijibu kwa kutingisha kichwa chake, akiashiria kukubaliana na mimi kwa kitu ambacho nimekizungumza.Nikanyanyuka kwenye benchi na kumshika mkono daktari na kumtanguliza mbele, akatoa simu yake mfukoni na kupiga sikujua anazungumza na nani
“Wee Merry maiti ya mgonjwa mumeiweka wapi?”
“Sanduku namba”
 
“Ahaa sawa, tangulia mochwar sisi tunakuja”
Akakata simu na kuidumbukiza kwenye mfuko wake wa koti alilo livaa, tukazidi kupigahatua za haraka hadi kwenye jengo la kuhifadhia maiti, nililo toka muda mchache ulio pita.Nikakuta nesi wawili wakiwa wamesimama nje ya mlango wa chumba cha maiti pamoja na mzee mmoja aliye valia mavazi meusi mkononi mwake akiwa ameshika jitochi kubwa
“Mbona kunagiza?”
“Daktari aliuliza?”
“Umeme umekatika, kuna shoti imetokea muda mchache ulio pita”
Mzee alijubu
“Ila maiti ya yule msichana muliiweka?”
“Ndio, tuliiweka”
Nesi mmoja alijibu, macho yangu yakatazama pande zote za eneo la jumba la kuhufadhia maiti, nilipo ridhika kwamba kina Regina  hawapo, nikaanza kutangulia kuingia ndani
“Ahaaa wewe kaka subiri mlizi atangulie na tochi”
Nesi mmoja alizungumza huku akiniwahi kunishika mkono
“Giza halina maana mbele ya mke wangu”
 
Nilizungumza kwa sauti nzito huku nikiutoa mkono wa nesi ulio nishika, mlinzi ambaye ndio yule mzee aliye valia nguo nyeusi, akafwatia kwa nyuma huku akimulika mulika kwenye madroo ya sehemu zilipo hifadhiwa maiti.
“Muliseme droo namba ngapi?”
Daktari aliuliza
“D-210 ipo kule mwisho”
Tukaelekea sehemu zilip droo, aliyo zungumza nesi, katika sehemu ambayo muda mchache nilikuwa na kina Regina haina uchafu wa aina yoyote na haionyeshi kama kuna tukio lolote lilifanyika siku hiyo.Mlizi akavuta droo alilo alekezwa na manesi hawa, ambao ninashangaa wana ujasiri mkubwa kama wanaume.Macho yetu tote yakatua kwenye sura ya binti mmoja ambaye sote hatukumtambua
“Mmmm”
Nilisikia mguno mmoja ukitoka kwa nesi aliye alekeza sehemu alipo tuagiza tufungue droo
“Nini?”
 
Doktar aliuliza kwa mashangao
“Mbona siye?”
“Muna uhakika mumemuweka humu?”
“Dokta sisi tunauhakika tumemuweka humu, si yule dada wa kiharabu?”
“Ndio, au mumekosea?”
“Dokta hatujakosea, mimi ndio nilikuwa mtu wa mwisho kulisukuma hili droo, au mlinzi ninakosea”
“Kweli hata mimi mwenye ninashangaa”
“Sikieni nyinyi musiniletee ujinga mke wangu, yupo wapi?”
“Kweli kaka yangu mkeo tulimuweka huku”
Gafla tukasikia mtikisiko wa kabati moja lililopo upande wa pili, sote tukakaa kimya, mtikisiko huo upo kama kuna mtu aliye zinduka kutoka katika usingizi mzito na kujikuta yupo ndani ya eneo hilo.
 
“Shiii”
Niliwaonya wasizungumze chochote, nikaanza kupig ahatua za kuelekea lilipo sanduku alinali kurupuka, nikawatazama daktari na wezake kila mmoja akaonekana kuwa katika hali ya mshangao, huku mlizi mikono yake ikitetemea hadi tochi aliyo ishika mwanga wake ukaanza kucheza cheza.Nikafika kwenye droo, kabla sikaulifungua moshi ukaanza kutoka kwenye droo hilo, huku likizidi kutetemeka.
Kwa ujasiri mkubwa nikaupeleka mkono wangu hadi kilipo kishikizo cha kisanduku, na kulivuta taratibu, kabla sijamalizia kulifungua, nikastukia kitu kikianguka nyuma, ilanilazimu kugeuka haraka na kukuta tochi ya mlinzi ikiwa imeanguka na kusababisha mwanga wake kupiga katika sehemu nilipo simama huku ukitokea chini.Macho ya daktari na manesi yakaanza kushangaa sana
 
“Nini mbona munashangaa?”
Niliwauliza baada ya kuona mshangao wao unazidi, kidole kimoja cha nesi mmoja kikaniashiria nigeuke nyuma yangu kuangalia kitu kinacho toka kwenye droo nililo lifungua.Nikageuka kwa haraka, sikuamini macho yangu, hii ni baada ya kukutana na mtu niliye fanana naye kuanzia juu hadi chini, isitoshe nguo zake na zangu zimefanana sana, jambo lililo nistua kupita maelezo.Akaanza kupiga chafya nyingi, nikastukia kishindo nyuma yangu, nikageuka na kumkuta nesi mmoja akiwa ameanguka na kupoteza fahamu huku mlinzi naye akifwatiakuanguka na kukaa kimya
“Mambo Eddy”
Jamaa alinisalimia, na sauti yangu inafanana sana na sauti yangu, nikabaki mdomo wazi nisijue nini nimjibu
 
  ITAENDELEA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya