Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya
chama cha ACT Wazalendo na Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Zitto Zuberi
Kabwe amemshukia Rais Magufuli baada ya kada wa chama hicho kutumbuliwa
siku chache baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Tarime.
Hidaya Usanga ambaye ni kada wa ACT
Wazalendo alikuwa pia mgombea ubunge katika jimbo la Malinyi mkoani
Morogoro, uteuzi wake ulitenguliwa mara moja na Rais Magufuli kwa kile
kilichoelezwa kuwa ni sababu za kichama.
Zitto Kabwe amehoji kauli ambazo Rais
Magufuli huwa akizinadi mara kwa mara kuwa anachagua watendaji wa
serikali kuangalia uchapakazi na si uchama sasa kwanini Hidaya
ameondolewa katika nafasi hiyo?
Rais Magufuli amekuwa akisema kuwa
maendeleo hayana chama na kuwa sote tunawajibu wa kushirikiana bila
kujali chama wala dini wala kabila, lakini leo Rais anamtumbua mtu kwa
sababu si kada wa CCM, hii inaonyesha kuwa anayoyazungumza Rais Magufuli
hayaamini, alisema Zitto Kabwe.
Zitto alihoji sababu ya nafasi za
utendaj serikali kupewa makada wa CCM, na alieleza Ikulu hawapo makini
katika teuzi wanazozifanya kwani hii si mara ya kwanza hizi teua, tumbua
zinatokea na kuwa tangu kwenye uteuzi wa wakuu wa wilaya, mikorogo
imekuwa mingi.
Hadi sasa hakuna taarifa rasmi kutoka Ikulu kuhusu kutenguliwa huko kwa Hidaya Usanga.
Post your Comment




