Hamissa Mobetto ni staa pekee wa Tanzania aliyetajwa kuwania tuzo za Starqt zinazofanyika nchini Afrika Kusini.
Mrembo huyo ametajwa kuwania vipengele viwili; Best Dressed Lady na People’s Choice Awards.
Hii ni mara ya tatu tuzo hizo zinatolewa na huwatunuku mastaa wa
Afrika kwa kazi wanazozifanya katika sekta za muziki, filamu, mitindo,
michezo na zingine.“Ni kitu kikubwa, somehow kinakuwa kama kinakutikisa kidogo hivi kiakili
kwasababu ukiwa mtu pekee kutoka kwenye nchi yako na mwanamke na
unakutana na watu wengine, lakini kila kitu kitakuwa kheri na tuzo
itarudi nyumbani,”Alisema Hamisa
“Mimi ni Mtanzania pekee niliyepo kwenye hizo tuzo na nilichaguliwa
na wao wenyewe wakaamua kuniweka kwa kuona ninafaa, kwasababu mnakutana
na watu wa Kenya, South Africa, Uganda, na nchi nyingine mbalimbali.
Kwahiyo kuwekwa tu pale inaonesha wanakuappreciate,” ameongeza.
Mrembo huyo amewaomba mashabiki wake kumpigia kura kwa kwenda kubonyeza link iliyopo kwenye bio yake ya Instagram.
Tuzo hizo zitatolewa September 10 nchini Afrika Kusini.
Post your Comment





