Mr Blue amekiri kuwa skendo yake kuwa amekuwa akiwasiliana na ex wake,
Naj ambaye kwa sasa ana uhusiano na Barakah Da Prince ilitaka kuivunja
ndoa yake.
Akiongea na Clouds FM, rapper huyo wa ‘Mboga Saba’ amedai kuwa mke
wake, Wahyda sasa amekuwa na wivu wa kufa mtu tangu kuzuke skendo hiyo.
“Sasa hivi naona kama wivu umezidi baada ya hii skendo ya hawa jamaa
kuitengenezea kiki kwasababu wanataka kutoa nyimbo yao, skendo kwamba
mimi nilimpigia yule mwanamke mwingine nani anaitwa, Najma yule.
Wametengeneza kweli kabisa, mimi nimezipata za kunyapianyapia kwamba
wametengeneza ili kukikisha nyimbo zao,” amesema Blue.“Lakini wamenikosea sana kwasababu wanataka kugombanisha ndoa yangu,
mimi nina mke ujue, siwezi kumpigia mtu ambaye nimemwacha, ni kosa kubwa
sana, halafu mke wangu yule ni mwanamke ambaye walikuwa watatu
kupigania nani awe na mimi, yaani bora hata ningempigia mtu mwingine,”
amesisitiza.
“Ilifika karibu kama siku mbili tuna ugomvi mimi na mke wangu, ni
kitu kikubwa sana, nimekasirika sana, nimechukia sana na nawaambia
mashabiki wangu, alichokifanya Barakah na watu wake, kama sio yeye
simlaumu, kama watu wake nilikuwa naomba waoneshe proof kwenye mitandao
waoneshe namba yangu niliyompigia, waioneshe kwamba ni hiyo kweli sio
unaongeaongea tu.”
Skendo hiyo ilianza baada ya Barakah kudaiwa kushika simu ya mpenzi wake Naj,
alipiga mtu ambaye namba yake ‘iliseviwa’ Zai na baada ya Barakah
kupokea alikuta sio mwanamke bali ni mwanaume ambaye alidaiwa kuwa ni Mr
Blue.
Post your Comment



