Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Handeni, anaye kaimu Ukuu wa Mkoa wa
Tanga kwa sasa, Mh Godwin Gondwe alipotembelea kambi tiba ya GSM
Foundation yenye lengo la kuokoa watoto zaikai ya 3500 wanaodaiwa
kupotea maisha kila mwaka kutokana na kuzaliwa na tatizo la kichwa
kikubwa na mgongo wazi.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Godwin Gondwe ambaye pia ni Mkuu
wa wilaya ya Handeni,Godwin Gondwe akigawa fedha za nauli kwa mmoja kati
ya wakazi wa wilaya hiyo Mwajuma Rashid ambaye ni mkazi wa Kijiji cha
Mkaramo wilayani Handeni mara baada ya kufika kwenye hospitali ya Mkoa
wa Tanga Bombo.
Gondwe aliipongeza taasisi inayojihusisha kusaidia sekta ya Afya na
Elimu hapa nchini kwa kutoa matibabu ya upasuaji huo kwa watoto hali
ambayo itawasaidia kuweza kurejea kwenye hali zao za kawaida.
Alisema katika suala kama hilo jamii haina budi kuacha kuwaficha
watoto wenye matatizo hayo badala yake waona namna ya kuwasiliana na
viongozi wao ngazi za chini kuwaepusha na vifo ambavyo vinaweza
kuwakumba kutokana na hali walizonazo.
“Lakini pia lazima jamii ibadilike kuona umuhimu wa kuacha kuwaficha
watoto wenye matatizo hayo badala yake wawapeleke kwenye hospitali
zilizopo karibu nao kwa ajili ya kupatiwa matibabu ambayo yatawasaidia
kupona “Alisema.
Akizungumza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo wakazi
wa zoezi la Upasuaji wa watoto hao lilipokuwa likiendeshwa na madaktari
Bingwa, Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji ya
(MOI)iliyopo Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili, Dkt Othman Kiloloma
alisema ongezeko la watoto hao linatokana na ukosefu wa lishe yenye
virutubisho vijulikanavyo kwa jina la “Folic Acid”
Alisema kukosekana kwa lishe hiyo kumesababisha tatizo hilo kwa
watoto ambalo lisipopatiwa ufumbuzi wa kina linaweza kupelekea athari
kubwa kwao ikiwemo vifo hali inayoweza kupunguza jamii ambayo ingeweza
kuchangia ukuaji wa uchumi katika shughuli za uzalishaji.
“Ukiangalia kwa hivi sasa zaidi ya watoto wapato 4000 wenye vichwa
vikubwa na mgongo wazi huzaliwa kila mwaka nchini na wanaoripotiwa
hospitalini si zaidi ya 500 hatua ambayo imechangia kwa asilimia kubwa
ongezeko la watoto wenye mtindio wa ubongo huku baadhi yao wakipoteza
maisha kwa sababu ya kukosa hivyo jamii inapaswa inapaswa kuwapeleka
katika Hospitali ili kuweza kuchangia ukuaji wao na maendeleo “Alisema
Kwa upande wa Afisa Habari wa Taasisi ya Afya inayojihusisha na
Upasuaji wa watoto hao, Khalfani Kiwamba alisema kuwa upungufu wa
madaktari wenye taaluma ya upasuaji wa waathirika hao ni mkubwa kwa
sababu nchini wapo saba ambapo sita wapo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
na mmoja yupo hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Bugando
Kufuatia hatua hito, Viongozi wa Taasisi za dini nchini zimeshauriwa
kuwahamasisha waumini wao wenye watoto wa aina hiyo kuwafikisha katika
Hospitali kubwa za Rufaa ili waweze kushauriwa badala ya kuwaficha
watoto hao majumbani ambapo wanapofikisha miaka kumi na kuendelea
uwezekano wa kupoteza maisha ni mkubwa sana.
“Kwani hatua hiyo imechangia kwa asilimia kubwa ongezeko la watoto
wenye mtindio wa ubongo huku baadhi yao wakipoteza maisha kwa sababu ya
kukosa tiba ,“Alisema
Post your Comment



