Nyota wa Bongo Fleva kutoka jijini Mwanza MO Music amefichua sababu ya
kundi la Wazawa, na kueleza kuwa ugomvi binafsi wa T Nocks na Baraka The
Price ndiyo uliopelekea kundi hilo kuvunjika.
Mo
Music alikuwa ni memba wa kundi hilo lililokuwa likiundwa na wasanii
kutoka lililojulikana kwa jina la WAZAWA, lililokuwa likiundwa na yeye
(MO Music), Baraka The Prince pamoja na T Nocks.
Mo aliongeza kuwa "Kila mtu ana akili zake tofauti na utofauti huo
ndiyo uliopelekea Wazawa kushindwa kudumu, mara nyingine miongoni mwetu
wengine walikuwa wanajiona bora zaidi ya wengine".
Pia Mo Music aligusia kwa kusema sababu ya ugomvi wa Baraka na T
Nocks kuwa ni wimbo wa So Fly, wimbo ambao ulimtambulisha Baraka vizuri
hasa kwa mkoa wa Mwanza.
Post your Comment



