Mtangazaji wa kituo cha runinga cha Channel 10, Cassius Mdami amefariki
dunia Jumatano hii mchana katika hospitali ya Mazimbu mkoani Morogoro.
Cassius aliugua ghafla kabla ya kufariki mkoani humo ambapo alikuwa
kwenye mapumziko yake mafupi mjini humo ambapo ndipo yalipokuwa makazi
yake ya muda mrefu.
Mwandishi huyo enzi za uhai wake amefanikiwa kuipata heshima kubwa
kituo chake cha runinga cha Channel 10 kupitia kipindi chake cha Utalii
Tanzania ambacho kilifanikiwa kupata tuzo kadhaa kutokana na
uhamasishaji wake kwenye sekta hiyo ya utalii.
Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi majira ya saa tisa
nyumbani kwake mkoani Morogoro. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Cassius
Mdami mahali pema peponi. Amina.
Post your Comment



