Nuh Mziwanda amesema wimbo wake Jike Shupa aliomshirikisha Alikiba,
umekuwa na mafanikio makubwa kuliko zote alizowahi kufanya huku video
yake ikiwa imetazamwa kwa zaidi ya mara milioni moja na laki tatu.
“Wimbo huu umeniletea mafaniko makubwa kuliko nyimbo zangu zote nilizoweza kufanya,”alisema Nuh.
“Pia tayari nina studio yangu ambayo ndio kitendo kikubwa katika
maisha yangu nilikuwa na kitaka kuna mchango pia wa kaka yangu katika
hii studio nawaza pia kuja kuwa na wasanii wangu, producer atakuwa ni
Nusder ambaye ameshafanya nyimbo nyingi,” aliongeza.
Post your Comment



