Msanii wa nyimbo za asili Saida Karoli aliyevuma kitambo, amefunguka na
kusema kuwa kitendo cha msanii Diamond Platnum kurudia moja ya kazi yake
anajihisi kuzaliwa upya.
Saida Karoli ambaye aliwahi kufanya vizuri na nyimbo kama ‘Mapenzi
kizunguzungu’, Kaisiki, Maria Salome na nyingine kibao na alifanikiwa
kuliteka soko la Afrika Mashariki kwa nyimbo hizo na kujipatia umaarufu
mkubwa mwanzoni mwa miaka ya 2000.
Saida Karoli amesikika kwenye moja ya clip ambayo ameiposti Diamond
Platnumz kwenye mitandao yake ya kijamii na kusema kuwa mwanzoni
waandishi wa habari walisha msahau walikuwa hawamtafuti tena, lakini
hata baadhi ya watu pamoja na ndugu zake walikuwa wakiambiwa kuwa
amekufa lakini baada ya kazi ya Diamond Platnumz kutoka imerejesha watu
kwenye himaya yake kwani wameanza kumtafuta na kumpigia simu sana.
“Mimi nimejisikia vizuri maana hii kazi tunayofanya ni kwa ajili ya
mashabiki, mashabiki ndiyo wadau wetu wanaotufanya sisi tuwe juu kwa
hiyo si kazi ya kwangu mimi peke yangu, ila mimi kama mimi nimejisikia
vizuri kusikiliza kwa sababu hata vyombo vya habari vilinisahau leo hii
vinanitafuta, haya ndugu zangu baadhi na wengine wanajua hata siko
duniani wanajua nilishakufa lakini leo hii naona watu mbalimbali
wananitafuta kweli nimefunguka najihisi kuzaliwa upya” alisikika Saida
Karoli
Post your Comment



